December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watakiwa kutumia taaluma kujinufaisha

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online,Dar

Diwani wa Kata ya Ilala na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya uchumi na huduma za jamii Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Saad Kimji,amesema watashirikiana ili kuondoa changamoto mbalimbali zinazokikabili chuo cha Amana Vijana Center.

Hivyo amewataka wahitimu kutumia vema taaluma waliyoipata chuoni hapo ili iweze kuwanufaisha huko waendako.

Akizungumza jijini Novemba 7, 2024, Kimji mbaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya wahitimu wa gani mbalimbali zinazotolewa chuo katika chuo hicho,ambapo amesema uongozi wa chuo cha Amana umefanya kazi ya kizalendo kwa utoaji wa kozi wezeshi ambazo ni muhimu kwa jamii ya Watanzania.

Hata hivyo kutokana na changamoto ya ajira Diwani huyo amesema kwa wale waliochukua kozi za hoteli ataongea na wamiliki wa hoteli waliopo maeneo hayoili waweze kuwapatia nafasi vijana waliohitimu kutoka chuo hicho.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo cha Amana Vijana Center Philipo Ndokeji,amewataka wahitimu hao wazingatie nidhamu na waendelee kufanya bidii katika maeneo wanaofanya kazi kwa vitendo (field).

Mmoja wa wahitimu wa fani ya hoteli Loveness John,amesema atatumia vema taaluma aliyoipata chuoni hapo katika kuendeleza familia yake pamoja na vizazi vingine vilivyoko karibu naye.