Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar es Salaam
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limewataka watu na Makampuni yenye uwezo wa kusafirisha Korosho nje ya Nchi kupitia Bandari ya Mtwara.
Wadau hao wanatakiwa kujitokeza kuomba vibali vya usafirishaji kutokana na Serikali kufanya maboresho makubwa katika bandari hiyo kwa sasa.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa (TASAC), Kaimu Mkeyenge, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, kuhusu upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu Kwa madai kuwa Wizara ya Uchukuzi kupitia shirika hilo inazuia watu wanaotaka kusafirisha Korosho nje ya Nchi kupata vibali.
“Bandari ya Mtwara ni Bandari muhimu sana na kumefanyika maboresho katika Bandari hii na imeonekana ni fursa kubwa sana ya usafirishaji wa korosho kutoka ndani ya nchi kwenda nje.
“Shirika tayari limetoka leseni kwenye kampuni yaliokidhi vigezo na zinaendelea na kazi, hivyo ningependa kutoa wito kwa wengine kuomba vibali na kama watakuwa wamekidhi vigezo basi watapatiwa,”,amesema Mkeyenge.
Amesema, tangu wameanza kutoa Vibali hivyo hadi kufikia Novemba 3, mwaka huu, tayari Makampuni 207 yamepewa Leseni ambapo tani zaidi ya 5,300 zinatarajiwa kusafirisha nje ya Nchi.
Aidha, TASAC imesema itaendelea kutekeleza maagizo ya Serikali pamoja na kusaidia Wananchi kwa ajili ya manufaa ya Taifa.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi