May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JWT yaanza ziara Pwani

Na Mwandishi Wetu, Pwani

JUMUIYA ya Wafanyabiasha nchini (JWT) imeanza ziara ya kikazi ya kusikiliza kero za wafanyabishara katika wilaya zote za mkoa wa Pwani,lengo ikiwa ni kusikiliza kero za wafanyabishara, wenye viwanda na kampuni ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu na kuepuka changamoto ikiwamo migomo ya mara kwa mara.

Akizungumza leo Mwenyekiti wa JWT, Hamis Livembe, akiwa ameongozana na viongozi wengine wamewasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kufanya mazunguzo na Katibu Tawala, Rashid Mchatta kabla ya kuanza mikutano yao.

Mwenyekiti huyo amesema Rais Samia Suluhu Hassan anawapenda wafanyabishara ndio sababu amewaagiza wasikilize kero zao na kuzipatia ufumbuzi wa kudumu.

Amesema wafanyabishara wakiungana wanaweza kujisemea na kumaliza kero zao bila kufunga biashara wala kufanya vurugu hivyo ni muhimu kujitokeza kwenye mikutano hiyo.

Aidha, Mchatta ameipongeza Jumuiya hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuisaidia serikali kusikiliza kero hizo nchi nzima na kuzifikisha kwenye mamlaka husika.

“Niwasihi tu viongozi wa JWT msiache kuwaelimisha wafanyabishara umuhimu wa kulipa kodi pamoja hayo wazingatie tahadhari za mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini,” amesema.