Na Sophia Fundi, Timesmajira Online,Karatu
Wananchi wilayani Karatu mkoani Arusha wameshauriwa kupambana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi ikiwa ni pamoja na kupima afya zao mara kwa mara ili kijikinga na mambukizi hayo.
Kauli hiyo imetolewa Desemba Mosi mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela wakati akizungumza na wananchi katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyo fanyika kimkoa katika viwanja vya mazingira bora wilayani Karatu ambapo amesema ni muhimu mtu kupima afya mara kwa mara ili kujikinga na maambukizi hayo.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema serikali inafanya kazi kubwa katika kupambana na maambukizi ya UKIMWI kwa kutoa elimu,dawa za kutosha kwa wale ambao wanaishi na maambukizi huku akisisitiza kuwa kupata maambukizi ya VVU sio mwisho wa maisha.
Amewapongeza wananchi kuacha kuwanyanyapaa waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI.
“Sasa hivi kwenye maeneo yetu hakuna ile tabia ya kuwanyanyapaa wagonjwa wa UKIMWI, jamii imeona kama ni ugonjwa wa kawaida nawapongeza sana wananchi,”amesema Mongela.
Amewaomba wadau kuendelea kushirikiana katika mapambano dhidi ya UKIMWI Kwa kutoa elimu ,kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujua afya zao ili kupunguza maambukizi au kumaliza kabisa.
“Ikumbukwe kuwa kila ifikapo tarehe Moja Desemba ya kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya UKIMWI duniani ambapo kwa mwaka huu imebebwa na kauli mbiu isemayo jamii iongoze kutokomeza UKIMWI.
More Stories
Sita wafariki kwa kipindupindu,wagonjwa 441 waripotiwa
DC Mgomi ataka wahitimu Jeshi la Akiba kuwa macho ya Serikali
Viongozi,Makada CCM kufanya ufunguzi kampeni Serikali za Mitaa