December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watahiniwa 877 Ilemela waanza mtihani kidato cha sita

Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza

Mtihani wa kidato cha sita (ACSEE) 2024 umeanza Leo Mei 6 hadi Mei 24,2024 nchini kote huku watahiniwa 877 waliosajiliwa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wanungana na wenzao kufanya mtihani huo kati yap wavulana ni 267 na wasichana ni 610.

Ambapo watahiniwa 822 ni wa shule wavulana 225 na wasichana 597 kati yao mtahiniwa mmoja (ke) ni mwenye uoni hafifu huku Watahiniwa 38 ni wa kujitegemea kati yap wavulana 32 na wasichana 6 na watahiniwa wa ualimu ni 17 kati yao wavulana 10 na wasichana 7.

Hayo yameelezwa Mei 6,2024 katika taarifa ilioyolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Violencea Mbakile,ambapo ameeleza kuwa mtihani huo wa kidato cha sita 2024 katika Halmashauri hiyo utafanyika katika vituo 10.

Ambapo kati ya hivyo vituo 8 ni vya shule, kituo kimoja cha kujitegemea huku kituo kimoja ni cha ualimu.

“Mkurugenzi wa Halmashauri Ummy Wayayu watahiniwa wa mtihani wa kidato cha sita na amewataka kufuata taratibu zote za mitihani na kuepuka udanganyifu huku amewatakia kila la kheri kwa kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu waanze na kumaliza salama mitihani,”ameeleza Mbakile.