Mtihani huo ambao umeanza leo Novemba 17
Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Jumla ya watahiniwa 7912 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2025 katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,wameungana na wanafunzi wengine nchini kote kuanza rasmi mtihani huo utakaofanyika kwa wiki mbili kuanzia leo Novemba 17 hadi Desemba 5,mwaka huu.
Kati ya watahiniwa 7912, 7691 ni watahiniwa wa shule ambao wavulana ni 3695 na wasichana ni 3996) na upande wa watahiniwa binafsi ni 221 ambao kati yao wavulana ni 106 na wasichana ni 115).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Ummy Wayayu,ametoa rai kwa wazazi kuhakikisha wanawasimamia watoto wao ili waweze kufanya mitihani yao kikamilifu.
Pia amewaasa watahiniwa wote kuepuka aina yoyote ya udanganyifu kwani wameandaliwa kikamilifu sambamba na kufuata taratibu, miongozo na sheria zote za mitihani.
Hata hivyo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ina jumla ya vituo 66 vya kufanyia mtihani, kati ya hivyo vituo 55 vikiwa ni vituo vya shule na vituo 11 ni vya watahiniwa binafsi.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako