Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
Utafiti wa Chuo Kikuu cha Washington, Marekani umebainisha kuwa, idadi ya watu watakaofariki kwa maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) hadi kufikia mwezi Agosti, mwaka huu itakuwa zaidi ya 145,000 nchini humo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na Shirika la Habari la Reuters kupitia ripoti ya watafiti katika Chuo Kikuu cha Washington nchini Marekani.
Kwa mujibu wa watafiti hao, idadi ya vifo hivyo huenda ikaongezeka zaidi kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.
Aidha, Taasisi ya Tathmini ya Afya ya chuo hicho cha Washington Ijumaa iliyopita pia ilitabiri kuwa idadi ya watu watakaofariki nchini Marekani hadi kufikia mwezi Agosti, mwaka huu itafikia 140,496.
Tabiri zote hizo zimetolewa huku takwimu zilizotolewa na tovuti ya Worldometers zikionyesha kuwa, watu 113,061 watafariki kwa maambukizi ya corona nchini Marekani kati ya jumla ya watu milioni 2,260,597 waliopatwa na ugonjwa huo.
More Stories
CCM yatuma salam za pole kifo cha Baba Mtakatifu Francisko
Rais Samia aomboleza kifo cha Papa Francisko
Papa Francis afariki Jumatatu ya Pasaka akiwa na miaka 88