Judith Ferdinand, Mwanza
Katika kuhakikisha taifa linakuwa na wataalamu wenye ujuzi zaidi katika ujengaji wa meli,Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa.Makame Mbarawa, ameagiza watalaam watatu kuletwa katika ujenzi unaoendelea wa meli ya MV.New Mwanza Hapa Kazi Tu,ili waweze kujifunza.
Profesa Mbarawa alitoa agizo hilo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa meli hiyo unaofanyika katika eneo la Bandari ya Mwanza Kusini (Mwanza South), jijini Mwanza, amesema wataalamu watatu waongezwe kwenye mradi huo,ili wapate fursa ya kujifunza na kupata ujuzi na ubunifu.
Ambapo hali hiyo itasaidia hata wakitaka kujenga meli nyingine wasipate shida baaada ya wakandarasi na wahandisi wageni kuondoka.
Amesema,kwa sasa wanachelezo kubwa hivyo wakitaka kujenga meli nyingine na za nchi za jirani wanatakiwa kuwa na wataalamu wa kutosha.
“Kuwa chelezo kikubwa ni jambo jingine na kufanya kazi ni jambo jingine,tunatakiwa kuongeza wataalamu wa kuja kujifunza leo,tusisubili kesho,tukisubili kesho tutakuwa tumechelewa,tutakuwa na chelezo kikubwa lakini hatuna watu,nikiangalia hapa Luteni Kanali Mstaafu Mapunda aliyekuwa anatutembeza hapa yupo mmoja sasa, nimeisha toa maelekezo kwamba tuwalete wataalamu wengine watatu nimesikia kuna wawili wa JMT na mmoja wa kule Zanzibar wote waletwe hapa wajifunze,”amesema na kuongeza kuwa
“Tecnician(mafundi)wengine waje hapa wajifunze,tutakapomaliza meli hii tunataka kujenga meli nyingine kama hatuna watu kila kitu kitakuwa ni shida kwani welding( uchomeleaji)unaofanyika hapo siyo ya kawaida kuwa utafika mtaani na kuchukua tu,utaalamu wake umebobea,kwaio lazima tuwalete vijana wajifunze na kuja kufanya sekta hii kufanya kazi vizuri,”.
Sanjari na hayo amesema, wamejenga meli hiyo kwa ajili ya wananchi yenye uwezo wa kubeba abiria 1200 na tani 400 za mizigo yakiwemo magari.
Amesema ujenzi wa meli hiyo utakapo kamilika utabadili na kuboresha hali ya usafiri na kuliwezesha Ziwa Victoria kufanya vizuri kwenye sekta ya usafirishaji na usafiri wa majini.
“Namshukuru Rais Samia Suluhu Hassan,na serikali kuiwezesha Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi fedha kuhakikisha miradi ya kimkakati ukiwemo wa meli mpya inajengwa kwa kasi ile ile na kukamilika,nasubiria kwa hamu meli hii ya kisasa yenye vyumba maalumu vya viongozi itaisha lini wananchi wapande, wana uwezo wa kuchagua wapite nchi kavu au wapande meli kwenda Bukoba, lakini tusiweke kasi kubwa ili kuokoa gharama kwa sababu mafuta mengi yatatumika,”amesema.
Akifafanua juu ya suala la kuchelewa kwa ujenzi wa meli hiyo amesema ni kutokana na mambo ya msingi na ili meli ijengwe ilitegemea kukamilika kwa chelezo ambacho ni kikubwa chenye viwango na endelevu ambacho kitatumika kujenga meli zingine zikiwemo za nchi jirani.
Amekemea upotoshaji unaoenezwa na watu wasioitakia mema serikali kwani miradi yote inaendelea ukiwemo wa meli hiyo ambapo aliishauri Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) ili kuondoa sinto fahamu kwa wananchi ni kuwapa waandishi wa habari fursa ya kutembelea mradi huo kila baada ya muda mfupi ili waweze kufahamu maendeleo ya mradi ulipo fikia sanjari na elimu ya kuwajengea uwezo kuhusu mradi huo ili waufahamu na kuuandika vizuri hali itakayosaidia wananchi kuelewa na kufahamu nini kinaendelea .
“Mradi huu wa meli unajengwa kwa vifaa vya kisasa, hatuwezi kuutekeleza bila wao (waandishi wa habari) wapeni elimu wapate uelewa na uzoefu ili waiandike miradi yetu vizuri na wataongea vitu vya kuwasaidia wananchi,tusiwaache waandike wasivyovifahamu,” alishauri Waziri huyo wa Ujenzi.
Kwa upande wake, Meneja wa mradi huo, Mhandisi Vitus Mapunda,amesema mradi huo umefikia asilimia 55 ambapo wamewekeza nguvu kwenye kazi za ndani ili kati ya April na Juni mwaka 2022 meli ishushwe majini.
Pia wanafanya mazoezi ya uhakiki wa chini ya meli kwenye mifumo ya mitambo ( injini) inavyofanya kazi na matenki ya maji kwa kupiga picha za X-ray kubaini sehemu zenye makosa yasiyoonekana kwa macho ya kibinadamu kwa sababu chini kunahitaji maarifa makubwa.
“Tunapiga picha za X–ray kubaini makosa, tunafanya majaribio (test) kwenye matenki ya maji kuona kama yako sawa hayana mvujiko wowote unaoweza kuleta madhara na tufanya hivi kujihami kabla ya mvua ambapo zimebaki ghorofa za juu ambazo ni rahisi,hazina mitambo mingi ni bapa na zina uzito mdogo,”alisema Mhandi Mapunda.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amina Makilangi, alisema mradi huo haujawahi kusimama na kumshukuru Rais Samia kwa namna anavyojali miradi ya kimkakati kuhakikisha inatekekezwa na kukamilika kwa wakati.
More Stories
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni