Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe Januari 23, 2025 akiwa katika Kituo cha Operesheni ya Matukio ya Dharura ya Afya ya Jamii (EOC) Mkoani Kagera ameongoza kikao cha Wataalam pamoja na Wadau wa Sekta ya Afya chenye lengo la kujadili hatua zilizofikiwa kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Marburg ikiwa ni pamoja na kuboresha mikakati ya kupambana na ugonjwa huo.
Mnamo Januari 19, 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliutangazia Umma uwepo wa mgonjwa mmoja mwenye maambukizi ya ugonjwa wa Marburg katika Wilaya Biharamulo, Kagera.
Timu ya wataalam afya pamoja wa wadau wa Sekta tayari imeshaweka kambi maalum katika Wilaya hiyo kwa ajili ya utoaji wa huduma za Elimu, tiba na kinga kwa wananchi.
Ugonjwa wa Marburg huenezwa kwa haraka kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia majimaji au damu ya mtu aliye na virusi hivyo.
Dalili za ugonjwa wa Marburg ni pamoja na homa kali, kuumwa kichwa, kutapika au kutapika damu, kuharisha au kuhara damu, kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili .
Jinsi ya kujikinga na Marburg ni pamoja na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni mara kwa mara, kuepuka kugusa au kuosha maiti ya mtu aliyefariki na ugonjwa wa Marburg, kuepuka kula au kugusa mizoga, na kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono.
More Stories
Msigwa aagiza ukamilishwaji wa haraka nyaraka muhimu za uanzishwaji wa bodi ya Ithibati ya waandishi wa habari
Mikopo ya ZEEA yaanza kutolewa kidijitali, maofisa washauriwa kuwa makini
Serikali yaja na mwarobaini wa changamoto ya Kivuko Magogoni – Kigamboni