May 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wataalam Afrika Mashariki wajadili nishati safi ya kupikia jijini Arusha

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

Kongamano la kwanza la Nishati Safi ya Kupikia Afrika Mashariki linaendelea jijini Arusha.

Leo tarehe 7 Mei, 2025 ambayo ni Siku ya Pili ya Kongamano, Wataalam kutoka Tanzania, Rwanda, Kenya, Burundi, Uganda na Malawi wanaendelea na majadiliano kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mbinu bora za utekelezaji wa Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia, maarifa na kupata uzoefu jinsi kila nchi inavyotekeleza ajenda hiyo.

Majadiliano hayo pia yanaangazia masuala ya uvumbuzi wa teknolojia za Nishati Safi ya Kupikia na masoko.

Katika kongamano hilo Wataalam pia wamefahamu hali ya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika eneo la Afrika Mashariki, changamoto zilizopo, fursa na hatua za kuchukua ili kufikia malengo yaliyowekwa katika kila nchi.

j