Na Mwandishi Wetu,TimesMajira
KAMPENI maalumu ya Darling Hair maarufu kama Loyalty Program, imezidi kushika kasi huku wasusi mbalimbali nchini wakiendelea kunufaika kwa njia mbalimbali wakati program hiyo ikiadhimisha miaka miwili tangu kuanzishwa kwake.
Wasusi mbalimbali wakizungumza katika sherehe maalulu iliyofanyika Gongo la Mboto na kuwakusanya wasusi mbalimbali katika kuadhimisha miaka miliwi ya program hiyo, waliipongeza Darling Hair kwa kuwajali na kuwawezesha kiuchumi kwa kuwapa vifaa baada ya kujizolea pointi kutokana na kukusanya lebo za bidhaa za kampuni hiyo.
“Siku ya leo imekuwa muhimu sana kwetu kama wasusi kwa sababu tumekutana na kubadilishana mawazo, tumepata mafunzo na pia vifaa mbalimbali vya saluni kutoka Darling Hair. Kwa kweli hawa hawana mpinzani,” amesema Jackline Temba ambaye anamiliki saluni eneo la Kitunda Jijini Dar es Salaam.

Ametoa wito kwa wasusi ambao hawajajiunga na program hiyo ya loyalty kufanya hivyo ili nao wafaidike na wajinyanyue kiuchumi.
Naye Regina Filbert kutoka Kitunda amesema kupitia program hiyo wasusi wamejifunza mambo mengi kutokana na mafunzo ya mara kwa mara na pia wamejishindia zawadi nyingi katika miaka miwili ya kampeni hii.
“Binafsi kupitia kampeni hii nimeshinda viti, rollers na vifaa vingine baada ya kukusanya lebo hizi na kukusanya pointi zilizoniwezesha kushinda,” amesema.
Salumu Hamisi, maarufu kama DD kutoka eneo la Banana, amesema Darling Hair imekuwa familia kwa wasusi na imekuwa ikiwafuatilia kwa karibu mno ili kuhakikisha wanashugulikia changamoto zozote na wasusi wote wanafikiwa wakubwa kwa wadogo.

“Wamekuwa ni wasikivu sana na wanatufuatilia kwa karibu. Changamoto zetu nyingi tu wameshazishugulikia ndio maana bidhaa zao zinaendelea kuongoza sokoni,”ameongeza.
Ametoa wito kwa wasusi mbalimbali kuangalia vifaa wanavyohitaji na kujiunga na program hiyo ili washinde na kujiongezea mitaji ili wafanye boashara kwa wepesi.
Mwakilishi wa Darling Hair, Daniel Kisusange kutoka idara ya Masoko, amesema hafla hii iliwakutanisha wasusi kutoka Gongo la Mboto, Chanika, Pugu, Banana, Kitunda na maeneo mengine.

More Stories
Watumishi Hospitali Rufaa Mbeya wanunua mashine ya kudurufu nyaraka
TANESCO yatunukiwa Tuzo kutambua mchango wake
wanawake magereza wahimizwa kujenga uwezo , kutumia fursa kidijitali