Na Mwandishi wetu,Timesmajira
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Tanzania Bara Stephen Wasira amesema katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu Chama kitaendelea kushika dola kwa wingi wa kura na si mtutu wa bunduki.
Pia, amesema CCM imebeba maono na fikra za ukombozi na kwamba itaendelea kuwa wakili wa kuwatetea Watanzania.
Wasira aliyasema hayo leo Februari 10, 2025 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Busega mkoani Simiyu alipokuwa akielekea jijini Mwanza.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/3-5-1024x683.jpg)
“Katika uchaguzi mkuu mwaka huu CCM tutashinda maana hakuna wa kupambana na CCM. Mtaji wetu ni kushika dola na dola hatuishiki kwa bunduki bali tunaishika kwa kura na kura zinapigwa na wana CCM na wasio wana CCM,” amesema Wasira
Akieleza zaidi kuhusu uimara wa CCM amesema unatokana na muungano wa vyama vilivyoleta ukombozi wa nchi ambavyo ni TANU na Afro-Shiraz Party (ASP).
“Kwa hiyo wanachama na viongozi wa Chama tunabeba maono ya vyama vilivyopita na sisi ndio tunaendeleza kazi ya uhuru, kuleta mabadiliko katika maisha ya watu,” amesema.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/2-7-1024x683.jpg)
Kuhusu wagombea ndani ya Chama amasema tayari CCM imeshapata wagombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Rais Dk. Samia Suluhu Hassan), Rais wa Zanzibar (Dk. Hussein Ali Mwinyi) na Mgombea Mwenza (Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi).
More Stories
Shule ya Hollyland yafagiliwa ubora wa taaluma
Dkt.Kiruswa: Tanzanite kuuzwa ndani, nje ya Mirerani
Jamii yatakiwa kutafsiri maendeleo yanayofanywa na Rais