May 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wasomi watakiwa kuachana na dhana ya kuajiriwa

Na Queen Lema TimesMajira Online, Arusha

Wito umetolewa kwa wasomi wenye fani mbalimbali hapa nchini kuachana na dhana potofu ya kuajiriwa na badala yake waweze kubuni na kutengeneza ajira zao wenyewe kwa kuwa Tanzania ina nafasi kubwa sana ya ajira binafsi na sio ajira za kujiajiri.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa shule ya wavulana tengeru (Tengeru boys) pamoja na holy ghost Viziwi,Farther John Assay wakati akizungumza kwenye ibada ya shukurani kwa ajili ya matokeo ya kidato cha NNE na cha pili ya mwaka 2023.

Assey alisema kuwa inasikitisha Sana kuona asilimia kubwa ya wasomi wa nchi ya Tanzania wanafuzu katika masomo nafani mbalimbali lakini wanalalamika kuwa hawana ajira za kudumu hivyo wanajikuta wakiwa wamerudi kwenye wimbi kubwa la umaskini

Alifafanua kuwa Hali hiyo inaongeza wimbi kubwa la umaskini na kulifanya taifa kuendelea kuwa tegemezi kwenye mataifa duniani

“Inasikitisha kuona wasomi wanamaliza vyuo vikuu lakini hawana ajira hivi hizo ajira za kuajiri wasomi wote zitapatikana wapi kwanini rasilimali zilizopo zisitumike kwa ajira binafsi”

Katika hatua nyingine alisema kuwa wasomi nao wanatakiwa kuhakikisha kuwa sasa wanaachana na Ile dhana ya kusema kuwa kuna Kazi za wasomi na wale ambao sio wasomi

“Ukiangalia wasomi wengi hawana muelekeo wa maisha na hawajui wafanye nini ili kujiingizia kipato lakini vijana ambao sio wasomi wanafanya kazi zote na huwa hawabagui kazi na maisha yao yanaenda vyema na pia Wana maendeleo mazuri Sana kwanini kila kijana asiwe mbunifu hasa kwenye soko la ajira”aliongeza

Wakati huo huo aliwataka vijana hasa waliopo sekondaro kuhakikisha kuwa wanaanza kuandaa kazi za kufanya tena za kujiajiri na kuachana na tabia ya kuwaza zaidi kuajiriwa tena Serikalini.

Naye Padre Florence Mlayi kutoka katika shirika la roho mtakatifu alisema kuwapamoja na kuwa shule hiyo ya Tengeru Boys imekuwa ikifanya vema katika matokeo ya mwisho lakini bado wazazi Wana nafasi kubwa sana ya kuweza kuwasaidia watoto wao hasa kwenye sekta ya makuzi

“Leo tuna Ibada ya shukurani kwa kuwa wanafunzi wote wamefaulu vyema kwenye mithiani yao na hatuna Sifuri lakini isiwe kigezo cha wazazi sasa kuona kuwa hawa vijana wamekuwa tena bado nafasi ya wazazi ipo pale pale”alisema

Aliwataka vijana ambao bado wapo shuleni kuhakikisha kuwa wanasoma kwa bidii lakini kuhakikisha wanakuwa katika malezi mazuri ambayo Yana msingi mzuri wa Imani lakini maadili ya kitanzania.

Jumla ya wahitimu 129 waliofanya mthiani wa kidato cha nne mwaka 2023 walifanikiwa kufaulu kwa kiwango cha daraja la Kwanza huku kidato cha pili nao wakifanya vema wote Jambo ambalo liliweza kuwakutanisha vijana hao ,wazazi,walezi,kwenye hafla ya sherehe ya Ibada ya shukurani huku nao walimu,wafanyakazi waliochochea wanafunzi hao kufanya vyema nao wakipatiwa zawadi Nono.