
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha amapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amewajibu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho John Heche, waliozungumzia umri wake hivi karibuni.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mkoani Geita jana Januari 29, 2025, Wasira amesema umri wake hauathiri uwezo wake wa kufikiri wala kufanya maamuzi sahihi.
“Mimi nina umri mkubwa lakini akili ni za miaka 55. Heche (John) akitaka akaulize madaktari wa India na Muhimbili, wamesema nina akili safi kabisa. Gari ni injini, siyo bodi,” alisema Wasira huku akiwataka wapinzani wake kuzingatia hoja badala ya umri wake.
Wasira ametoa mfano wa @realDonaldTrump, ambaye amechaguliwa kuwa Rais wa Marekani katika uchaguzi wa hivi karibuni, akisema kuwa licha ya umri wake mkubwa, Wamarekani walimchagua kwa sababu ya sera zake na si kwa kuangalia umri wake.
“Heche akitaka ushahidi aende Marekani akawaulize wamarekani kwanini walimchagua Donald Trump mwenye umri kama wangu na wakamuacha Kamala Harris mwenye miaka 60,” alisisitiza Wasira.
More Stories
Kiongozi wa Mwenge awataka RUWASA kukamilisha mradi wa maji kwa wakati Kilindi
Balozi Nchimbi aongoza waombolezaji kumuaga Mzee Mongella
Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua mama yake mzazi