February 21, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wasira aihakikishia Marekani uchaguzi nchini kuwa wa huru na haki

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira amesema kipaumbele cha Chama wakati wote ni kuhakikisha nchi inakuwa na amani.

Pia, ameihakikishia kuwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu, utakuwa huru na wa haki.

Wasira amesema hayo leo Februari 20, 2025 alipozungumza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz, aliyemtembea ofisi kwake katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti Wasira alimweleza kaimu balozi huyo kwamba, Tanzania ni taifa linaloendelea, hivyo amani ya nchi haiwezi kuwekwa rehani.

Katika mazungumzo yao, wawili hao walizungumzia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini baadaye mwaka huu, ambapo Wasira alimhakikishia Lentz kwamba utafanyika kwa uhuru na haki.

Alimwambia Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kujiandaa kushiriki uchaguzi huo na kinatarajia kushinda kwa sababu kimetekeleza ahadi za maendeleo zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

Kuhusu swali la Kaimu Balozi Lentz kwamba je, CCM ipo tayari kuzungumza na vyama vya upinzani, Wasira alisema ipo tayari na ndiyo msingi wa falsafa ya R4 ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wasira alisema kuwa, R4 zinasisitiza mazungumzo pale ambapo kuna kutofautiana kimisimamo baina ya vyama.

Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti Wasira alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini, Yordenis Despaigne.

Makamu Mwenyekiti Wasira na balozi huyo walikubaliana kuendeleza urafiki na ushirikiano wa maendeleo katika nyanja mbalimbali ambao umedumu kwa muda mrefu tangu wakati wa utawala wa swrikali ya awamu ya kwanza chini Hayati Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Fidel Castro