Na Mwadishi Wetu, TimesMajira Online
WASHIRIKI wa miss Mwanza 2021 na uongozi wao wametembelea kituo chakulele watoto wenyewe uhitaji maalum Hisani Center, Buswera wilayani Ilemela na kushiriki nao michezo mbalimbali.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi, Mkurugenzi wa shindano hilo Sebastian Kaluguru amesema moja ya kazi ya warembo ni kuwa karibu na jamii na kutoa huduma husika kwa wale wanaohitaji.
“Leo tumekuja kutembelea watoto ambao wanaishi katika kituo hichi cha Hisani Center, pamoja na zawadi ambazo zitawasaidia katika maisha yao ya hapa nyumbani, hii itakuwa ni endelevu na tutatembelea katika vituo mbalimbali wakati huu wa kambi na baada ya kumaliza mashindano mshindi atakayepatikana ataendeleza mfumo huu,” amesema Kaluguru.
Hata hivyo, amesema jamii haipaswi kuwasahau watoto wanaoishi katika mazingira magum hivyo ameomba mashirika, taasisi na serekali kuwakumbuka mara kwa mara na kuunda kampeni pamoja na sera zitakazo wasaidi kujikwamua.
Kwa upande wake mlezi wa kituo hicho Grece Pita ameushukuru uongozi wa Miss Mwanza na kuwakaribisha watu ambao wana uwezo wa kuwasaidi watoto hao kwa upande wa chakula, elimu na afya na ushauri kujitokeza.
More Stories
Mzee wa Bwax afunika ‘Kitaa food Fest’ Mbagala
TBL yazindua Kampeni ya ‘Smart Drinking’
Msimu wa nne,tuzo za eagle entertainment, kufanyika kivingine