Na Penina Malundo,Timesmajira
KONGAMANO la Tano la Uongozi Wanawake lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi(Uongozi Institute)chini ya dhima ya Mchango wa wanawake katika uongozi barani Afrika limefanyika leo jijini Dar es Salaam na takribani washiriki kutoka nchi 16 ikiwemo Tanzania wameweza kushiriki.
Miongoni mwa nchi hizo zilizoshiriki ni pamoja na Kenya, Afrika ya Kusini, Rwanda, Gambia, Zambia, Nigeria, Liberia na mwenyeji Tanzania kwa kutaja chache.
Ameyasema hayo leo Oktoba 6,2025 katika ufunguzi wa Jukwaa hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi,Kadari Singo amesema washiriki hao ambao ni wanawake wamekutana kwaajili ya Jukwaa la Uongozi wa maendeleo endelevu kwaajili ya kuendeleza wanawake katika suala la Uongozi kwa Afrika.
Singo amesema lengo la Taasisi ya Uongozi ni kuwafikia wanawake viongozi barani Afrika katika kuhakikisha wanajengewa uwezo ili wanapochukua nafasi za uongozi waweze kutumikia vema.
”Takwimu zinaonesha kwamba mpaka sasa kuna asilimia 33 pekee yake wanaoshikilia nafasi kubwa za maamuzi duniani,kwa spidi hii inaonesha kuwa itachukua miaka 130 kufikia 50 kwa 50 kama spidi itakuwa haijaongezeka.

”Imekuwa jitihada za Taasisi ya Uongozi kuhakikisha kwamba wanaendelea kuwajengea uwezo wanawake wengi zaidi wenyesifa kushika nafasi ya uongozi barani Afrika,”amesema Singo
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt.John Jingu wakati akifungua jukwaa hilo amesema kuzinduliwa kwa programu hiyo itaweza kuwasaidia Wanawake hao ambao ni washiriki wa kongamano hilo kujengewa uwezo na kuja kuwa viongozi wazuri wenye mchango wa maendeleo ya jamii katika maeneo ambayo wapo.

”Jukwaa hili lililopo chini ya Uongozi Institute ni zuri sana linatoa fursa kwa washiriki ya kubadilishana uzoefu wao kwa wao,watu waliokuwepo katika nafasi ya uongozi.”Kila mmoja wa washiriki waliopo katika mafunzo haya nimeambiwa kuwa mnakuwa na walezi wenu katika maeneo mbalimbali,kama kwenye biashara au Serikalini,ili wawajengea uwezo sehemu ambazo mpo.”amesema
Amesema hatua hiyo itawasaidia kupata ujuzi na sifa zinazohitajika katika maeneo yao na sio nadharia ya kusoma vitabu pekee.
”Hapa tunatengeneza waleta mabadiliko,katika jamii yetu na tunakubaliana tukishiriki wote katika shughuli za maendeleo tutaleta mafanikio makubwa katika jamii yetu na kuwa na jamii iliyostawi na maendeleo endelevu.

Naye Balozi wa Finland nchini Tanzania,Theresa Zitting amesema uongozi sio juu ya nafasi bali ni juu ya wao wenyewe kuvumilia na kutoshindwa hivyo ni vema wanawake hao wasiogope kuanguka bali wasimame na kujaribu.
”Tunahitaji kuona ustahimilivu ili tusifeli kama tunaona tunaferi tunapaswa kusimama na kuendelea tena na tena,”amesema Zitting Ufunguzi wa Jukwaa hilo linafanyika kama sehemu ya Programu ya Uongozi kwa Wanawake (Women’s Leadership Programme) ya Taasisi ya UONGOZI, yenye lengo la kukuza nafasi za uongozi kwa wanawake.
Programu hii ya miezi sita inajumuisha kongamano, mafunzo ya mfululizo ya siku sita, pamoja na ushauri mahususi wa kukuza sifa za uongozi.

Utekelezaji wa programu hii unawezeshwa kwa kiasi kikubwa na Serikali ya Tanzania na Serikali ya Finland, pamoja na Umoja wa Ulaya.
Wageni watakaohudhuria ni pamoja na viongozi waandamizi kutoka nchi mbalimbali duniani na sekta zote ikiwemo sekta ya umma, sekta binafsi, sekta ya elimu ya juu, na sekta ya asasi za kiraia; pamoja na wanawake 100 waliochaguliwa kujiunga na Programu ya Uongozi kwa Wanawake.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako