December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Washindi kampeni ya Airtel waelekea kushuhudia fainali AFCON 2023

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dar es Salaam

HATIMAYE washindi wanne wa kampeni ya siku 90 iliyoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Airtel ikishirikiana na TECNO ya Upige Mwingi Mpaka AFCON, wameondoka kuelekea nchini Ivory Coast kwaajili ya kushuhudia fainali za mashindano ya AFCON 2023 yanaendelea nchini humo.

Washindi hao ambao ni Marcel Leonard, Jafari Salukele, Alfred Mlita, na John Kimario wameondoka nchini na kuagwa na Mkurugenzi wa Airtel Money jana usiku wa tarehe 8, huku ambapo watashuhudia fainali kati ya timu ya Nigeria ‘Super Eagles’ na nchi wenyeji ya Ivory Coast.

Akizungumza wakati wa kuwaaga washindi hao, Mkurugezi wa Airtel Money, Andrew Mugamba alisema kuwa promosheni hiyo inaonesha dhahiri jinsi Airtel Tanzania inavyojitolea kufikisha huduma nzuri kwa wateja wake pamoja na kuwapa kumbukumbu zisizosahaulika.

Pamoja na washindi hao wanne waliopatoikana katika kampeni hiyo, pia imetoa zawadi mbalimbali zikiwemo simu janja za TECHNo Spark 20, jokofu, TV, bodaboda pamoja na vifuruushi vya data, dakika na SMS kwa washindi mbalimbali walioshiriki nchini.

Andrew alisema, “Leo ni hatua muhimu katika safari yetu tunapowatuma washindi hawa kushuhudia soka la Afrika katika kilele cha AFCON 2023. Tunafuraha kuona washindi wetu wakianza safari hii kuelekea Ivory Coast na kufurahia soka la Afrika.”

Kwa upande wake Jafari Salukele ambaye ni mmoja wa washindi hao na mjasiriamali ameonesha furaha yake na kusema kuw anashukuru kwa fursa hii ya mara moja maishani kushuhudia fainali za AFCON 2024 moja kwa moja nchini Ivory Coast.

“Ni ndoto kutimia kwa shabiki yeyote wa soka kuwa mmoja wa waliobahatika kupitia promosheni ya ‘Upige Mwingi Mpaka AFCON’. Nashukuru sana Airtel Tanzania na TECNO kwa zawadi hii ya ajabu na kwa kufanya ndoto kama zangu kuwa ukweli” alisema Salukele.

Ushirikiano wa Airtel Tanzania na TECNO umekuwa muhimu katika safari hii, ukilenga kuongeza umahiri wa simu kwa bei nafuu na zenye ubora kama vile Tecno Spark 20 zipatikane kwa wateja kwa urahisi zaidi.

Ushirikiano huu unasisitiza zaidi maono ya pamoja ya kuvuka mipaka katika michezo na teknolojia, na kuwahimiza wateja wa Airtel kutimiza ndoto kubwa na kufikia uwezo wao kamili.

“Tunawahimiza wateja zaidi kushiriki katika ofa ya Upige Mwingi kwani kuna zawadi zaidi za kushinda.” aliongeza Bw. Andrew