Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
WASANII mbalimbali hapa nchini wameguswa vikali na
ajali ya moto iliyotokea usiku wa kuamkia leo kwenye
Soko Kuu la Kariakoo jijini, Dar es Salaam na ile ya
Bweni la Shule ya Sekondari ya Kiislam ya Wasichana AT
-TAUN inayomilikiwa na Taasisi ya Kiislam iliyopo mji
Mpya katika Manispaa ya Morogoro.
Wakitoa pole kwa waliokumbwa na mahafa hayo, kupitia
kwenye Kurasa zao za Instagrama wasanii hao wamesema
kutokana na matukio hayo mamlaka husika zitafanya kazi
yake ili kubaini chanzo.
Nandy
MSANII wa muziki wa Bongo fleva ambaye kwa sasa
anafanya vizuri katika Festival yake Faustine Charles
maarufu kama ‘Nandy’amewapa pole nyingi sana wafanya
biashara wote wa soko la Kariakoo kutokana na hali
iliyowakuta
“Moyo wa uvumilivu na subira viwe juu yetu. Hili janga
na Taifa Mungu Ibariki Tanzania,” ameandika Nandy
kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram.
Shilole
Naye msanii wa muziki wa Bongo fleva na Mjasiriamali
hapa nchini Zuwena Mohamed maarufu kama ‘Shilole’
amejawa na huzuni kufuatia wajasiriamali wenzake
waliopo sokoni Kariakoo kupatwa na mahafa.
“Natoa pole kwa wajasiriamali wenzangu wote
walioharibikiwa ama kupotelewa na mali zao sokoni
kariakoo, kutokana na moto uliotokea usiku wa kuamkia
jana. Naamini mamlaka husika inafanya kazi kubaini
chanzo, ili kuweka tahadhari madhira haya yasije
kutupata tena siku za mbeleni,” ameandika shilole.
Diamondplatnumz
Kwa Upande wake, Nyota wa Bongo fleva na Bosi wa Wasafi
Media Diamondplatnumz ameguswa na ajali ya Moto ambazo
zimetokea usiku wa kuamkia jana, Moja ikiwa ya Soko la
Kariakoo na ya Pili ikiwa Shule ya Sekondari ya Kiislam
Wasichana AT -TAUN inayomilikiwa na Taasisi ya Kiislam
iliyopo mji Mpya katika Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza kwa masikitiko kupitia kwenye Ukurasa wake
wa Instagram Diamond amesema, amepokea kwa masikitiko
makubwa kufuata kutokea kwa ajali hizo.
“Nimepokea kwa masikitiko Makubwa, ajali ya Moto
iliyotokea Morogoro na Sokoni Kariakoo.Mwenyezi Mungu
awatie nguvu Wafanyabiashara wote,pamoja na kila
aliyeguswa na ajali hii ya Moto, Mimi kama kijana wa
Kitanzania niko tayari kushiriki kwa hali na Mali
katika kurejesha faraja za ndugu zetu waliopatwa na
matatizo,” amesema Diamond.
Rosa Ree
MSANII wa muziki wa rap kwa upande wa wanawake Rosa Ree
naye ni miongoni mwa wasanii waliohudhunika na ajali ya
moto Sokoni Kariakoo iliyotokea usiku wa kuamkia jana
na ile ya Sule ya Kiislamu Morogoro.
“Mungu wangu, tunajua kwamba vyote vinavyotokea hua
sambamba na mipango yako. Basi waangalie hawa waja
wako. Watete hawa wanao Mungu wetu dah?.Poleni sana
ndugu zangu mliothirika na moto wa Kariakoo. Mungu
awape nguvu maana yake kila kitu kinawezekana,”
ameandika Rosa Ree.
%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%
More Stories
Mzee wa Bwax afunika ‘Kitaa food Fest’ Mbagala
TBL yazindua Kampeni ya ‘Smart Drinking’
Msimu wa nne,tuzo za eagle entertainment, kufanyika kivingine