December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wasanii wa filamu wamuunga mkono Diwani Kibaha

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

WASANII wa shirikisho la filamu Tanzania, wameungana na diwani wa viti maalum Kibaha, Lydia Mgaya kwa ajili ya kumuunga mkono kwenye ujenzi wa nyumba ya watoto yatima na wajane.

Hata hivyo, Wasanii hao ambao waliongozana na msanii mkubwa wa filamu, Hidaya Njaidi, wamesema watakuwa bega kwa bega na Lydia, kwasababu amekuwa mfano wa kuigwa kwa kujitolea kujenga nyumba hiyo maana angeweza hata hela yake angefanyia kitu kingine chochote.

Kwa upande wake diwani Lydia amesema, anawashukuru sana wasanii wenzake kwasababu wanamfanya azidi kupambana zaidi, maana wameonyesha wazi moyo wa upendo wa kutoka mbali na kuungana naye.