January 17, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wasanii wa ‘Comedy’ kuwania tuzo

Na Bakari Lulela,Timesmajiraonline,Dar

KWA mara ya kwanza katika historia ya Tanzania. Tanzania Comedy awards zimeziduliwa rasmi zikiwa na lengo la kutambua na kukuza mchango wa kazi za wachekeshaji katika tasnia ya sanaa nchini.

Uzinduzi huo umefanyika Januari 15,2025 katika hotel ya Johari Rotana jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya sanaa wakiwemo wachekeshaji maarufu.

Tuzo hizi zimeandaliwa kwa ushirikiano wa Baraza la sanaa (BASATA), Bodi ya filamu Tanzania na msanii mashuhuri wa Bongo Fleva Omari Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz.

Tukio Hilo limepata baraka kutoka kwa viongozi wa sekta ya sanaa wakiwemo Katibu mtendaji wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) Dkt.Kedmon Mapana ambaye alimpongeza Ommy Dimpoz kwa kuanzisha wazo Hilo lenye tija kubwa kwa wasanii wa tasnia ya vichekesho.

“Ommy Dimpoz alipokuja na wazo hili tulilipokea kwa mikono miwili kwa kuwa linaenda sambamba na dhamira yetu ya kuendeleza sanaa na wasanii wa Tanzania. Tuzo hizi sio tu umahiri wa kazi ya uchekeshaji nchini Bali pia zitaitangaza Tanzania kwenye medali za kimataifa,” amesema Mapana

Vipengele vya Tuzo na Zawadi kubwa
Tuzo hizi zinajumuisha vipengele 21 ikiwemo Comedian of the year,female comedian na Comedian of the month washindi wa Tuzo kubwa ambapo watapokea kiasi cha pesa kama Zawadi kama ifuatavyo
Mchekeshaji Bora wa kike Milioni 20
Mchekeshaji Bora wa kiume milioni 20
Mchekeshaji Bora wa mwaka milioni 30
Washindi wa vipengele vingine watapata milioni 5 kila mmoja.

Hafla za utolewaji wa Tuzo hizo zitafanyika Februari 14,2025 kushiriki kwa kuwapigia kura wachekeshaji wanaowapenda na kufanya hafla kuwa ya kipekee na kufana  katika ukumbi wa super Dome masaki jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake Omari Nyembo maarufu Ommy Dimpoz amesema aliamua kuanzisha Tuzo hizi kutokana na kutokuwa kwa jukwaa maalumu la kutambua mchango wa wachekeshaji nchini.

“Tuzo hizi ni hatua kubwa kwa tasnia ya burudani nchini ni wakati wa wachekeshaji kushiriki na kuwa sehemu ya historia kwa kushiriki katika Tuzo hizo ambazo zinakuza ubunifu na mashirikiano wasanii watanzania,”amesema Ommy Dimpoz

Usimamizi wa serikali
Uzinduzi wa Tuzo za Tanzania Comedian awards (TCA) umeratibiwa na Baraza la sanaa na Bodi ya filamu chini ya wizara ya utamaduni sanaa na michezo huku ukisimamiwa na Naibu waziri wa wizara hiyo Khamis Mwinjuma