December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

WasafiBet wazindua Promosheni ya Jipate na EURO 2024

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

KUFUATIA michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2024) inayotarajiwa kuanza Juni 14 mwaka huu nchini Ujerumani, Wasafibet wamezindua kampeni mpya ya ‘Jipate na EURO’ iliyoambatana na zawadi
mbalimbali kwa washindi wake.

Akizungumza na waandishi wa Habari mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Wasafibet, ambaye pia msanii wa muziki wa Bongo fleva, Naseeb Abdul maarufu kama ‘DiamondPlatnumz’ alisema kila wiki zawadi mbalimbali zitatolewa ikiwemo smartphone, smart tv,
bodaboda n.k.

“Sikuzote mteja ni mfale, hivyo tunamuwekea mteja zawadi ya Smart
TV, Bodaboda, Smartphone. Nawasihi wateja wote wacheze na WasafiBet ili
muweze kujishindia zawadi mbalimbali “

Kwa upande wake Balozi wa Wasafibet, Baba Levo alisema mchezo huo wa kubahatisha ni wa kuaminika na haugusi kwenye maisha ya kilasiku ya mteja, hivyo amewataka wateja wote kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kupata fursa ya kusafiri Ulaya.

“Sisi hatutaki watu wacheze hadi ela yake ya mwisho, ndiyo maana tunasema cheza kistaarabu, huu ni mchezo wa kawaida na haigusi kwenye maisha yako ya kawaida, sisi tunahudumia zaidi kuliko kutengeneza
faida,” alisema Baba Levo.

Baba Levo aliwasihi watu wote kujiunga na wasafi Bet ili kuwa katika watu ambao muda wowote watakwenda Ulaya.

“Tukisema watu wanaenda Ulaya wanaenda kweli Ulaya, watu wanabet
na WasafiBet, kama hauna App basi ipakue sasahivi ili uweze kufika Ulaya,” alisisitiza

Mbali na hayo, Taasisi hiyo ya Wasafibet
ilimkabidhi Said Daudi kutoka mkoani Tabora hundi ya shilingi Milioni Ishirini (20,000,000/-) kupitia kampeni ya Maokoto ya EPL 2023/2024.

“Wakati naanza mziki nilimwambia mama
yangu, nikiokota milioni Moja tu nitamuona Adam juma nitengeneze video ,nikapata milioni Moja nikatengeneza video na hadi sasa nimefika hapa.

“Hivyo hii milioni 20 uliyoipata ni kitu ambacho kitaongeza katika uwekezaji uliufanya au biashara unazozifanya tunaamini zitakuja kuzaa zaidi,” alisema Naseeb Abdul.

Naye Mshindi wa kampeni hiyo ya Maokoto ya EPL 2023/24, Daudi aliishukuru Taasisi hiyo ya WasafiBet kwa kuanzisha mchezo huo lakini pia kumpa ushindi huo na kuahidi fedha hizo kwenda
kuzitumia katika kuendeleza biashara zake.