Na Bakari Lulela, Timesmajira Online,Dar
Nyumba namba 384 iliyopo Tandale kwa Mkunduge jijini Dar es salaam,Januari 28,2025,majira ya saa mbili za usiku imepata hitilafu ya umeme na baadhi ya vyumba kuteketea kwa moto.
Tukio hilo lilizua taharuki kwa wapangaji na wakazi wa maeneo hayo, palitokea sintofahamu mali kuibiwa na watu ambao si wema lakini vingine viliteketea kwa moto.
Akizungumza katika eneo hilo mmiliki wa nyumba hiyo Kenneth Daniel,amesema hitilafu ya umeme ndio chanzo cha moto huo,ambapo nyumba yake ina vyumba kumi lakini vyumba vinne ndivyo vilivyo athirika na moto huo.
“Naiomba Serikali,inisaidie na kuwasaidia wapangaji walioathirika na moto, binafsi sikai hapa ila nilipata taarifa za tukio hili kwa kupigiwa simu, nami nilichukua jukumu la kuwapigia simu kikosi cha Zimamoto ambao hawakuweza kupokea,” amesema Danniel.
Daniel amesema kulingana na hali ya ugumu wa maisha inayoikabili jamii kwa sasa ameiomba serikali kuweza kumsaidia Ili kugharamia baadhi ya vitu vilivyoathirika ama kujenga miundombinu ya jengo hilo upya.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa mtaa huo,Ramadhani Mbaga, amesema wao kama Serikali wanaanza na utaratibu wa awali katika kuwasaidia waathirika hao, moja ni kuangalia thamani ya upotevu wa mali na kuwahifadhi.
Hivyo ametoa wito kwa wakazi wa mtaa huo kuwa na tabia ya kuwapeleka wataalamu wa mifumo ya umeme,ili kukagua ama kubadilisha miundombinu ya zamani ambayo ni chanzo cha matatizo mbalimbali .
Mmoja wa waathirika wa ajali hiyo, Habibu Abdallah,amesema kuwa ameathirika kwa asilimia kubwa ambapo vitu vingi vimeteketea kwa moto ikiwemo thamani ya fedha ya million 1.7 ambazo alikuwa amedhihifadhi kwa ajili ya mambo yake.
More Stories
Premium Active Tanzania yapunguza uhaba wa madawati Mlele
TARURA Kilindi kutumia bil.5.2 bajeti 2025/26
Madiwani Kilindi wapitisha bil.36.8 bajeti 2025/26