Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha
Wanawake nchini Tanzania wameshauriwa kujiwekea utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya zao hasa kwa kupima saratani za mlango wa kizazi,saratani ya koo pamoja na saratani ya Matiti Kwa kuwa bado kuna wanawake ambao wanapokabikiwa na saratani hizo
Aidha kwa Sasa ndani ya nchi ya Tanzania Kati ya wagonjwa 100 wagonjwa 47 wanakabiliwa na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi hivyo ni muhimu kupima afya mapema
Hayo yameelezwa na Dkt Maguha Stefano ambaye ni Meneja wa kinga kutoka katika taasisi ya Ocean Road wakati akiongea kwenye kambi ya madaktari Ambao walikuwa wanafanya uchunguzi wa awali wa saratani mapema Jana katika hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru.
Dkt Maguha alisema kuwa saratani ya mlango wa kizazi ni ya Kwanza ambapo saratani ya Matiti inashika nafasi ya pili ikifuatiwa na saratani ya koo
Alisema Kwa wanaume wanakabiliwa na saratani ya koo,pamoja na saratani ya tezi dume ambapo mpaka sasa jitiada za kufanya uchunguzi pamoan na kutoa elimu kwa jamii zinaendelea
“Ugonjwa wa saratani unatokana na mabadiliko ya chembechembe hai,unapokwenda kupata vipimo Kila mara unaweza kuisaidia kupata Tiba mapema Sana lakini ukichelewa kupata matibabu haya ya saratani basi unahatarisha maisha nawasihi Sana watanzania sasa wafanye vipimo vyao mara kwa mara Kwa kuwa hapo awali Kwa saratani ya mlango wa uzazi dalili hazioneshi mapema Ila ukifanya uchunguzi wa awali ni Raisi kuweza kujua” aliongeza
Aliongeza ugonjwa wa saratani ni ugonjwa ambao haumbukizi lakini ni muhimu sasa Kwa jamii kuhakikisha kuwa killa mara wanachukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kupata kinga
Alitaja baadhi ya sababu ambazo zinaweza kusababisha saratani ya mlango wa kizazi be kuwa ni pamoja na wasichana ambao wanafanya ngono wakiwa katika umri mdogo wanatakiwa kuacha kwani Tabia hiyo unaweza kuwaweka katika athari ambazo zinaweza kuwafanya kupata maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi
Aliendelea Kwa kusema kuwa sababu nyingine ambayo unaweza kusababisha saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na kufanya ngono na wanaume wengi Jambo ambalo ni hatari kwa afya ya mwanamke na huenda likasababisha saratani hiyo ya mlango wa kizazi
“Hizo ni sababu Tu mojawapo lakini pia kina sababu tena nyingine kama sababu ya uvutaji wa tumbaku na vitu vingine kama shisha nawasihi sana wanawake wasijiingize katika uvutaji wa sigara na vitu kama hivyo kwani si salama hata kidogo”aliongeza.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu