November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake walemavu wapewa simu kurahisisha mawasiliano

Mkurugenzi wa Elimu Maalum nchini kutoka Wizara ya Elimu, Magreth Matonya akimkabidhi simu kama kifaa kisaidizi katika mawasiliano kwa watu wenye ulemavu Mwenyekiti wa Wanawake na Watoto wenye ulemavu Tanzania, Nuru Awadhi. (Picha na Penina Malundo).

Na Penina Malundo Timesmajira Online

KUNDI la Wanawake Walemavu kutoka Jumuiya ya Wanawake ya Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata) na Taasisi ya Sauti ya wanawake Walemavu limekabidhia simu 30 ili kuwasaidia kwenye mawasiliano.

Mkuu wa Kitengo na Ufuatiliaji na Uthamini wa Shirika Kimataifa linalofanya watu wenye ulemavu la Add International, Shabani Abeid amesema, taasisi yao imeona ni jambo jema la kuwasaidia watu wa kundi hilo katika kuwarahisishia mawasiliano.

Amesema, simu hizo ni vifaa saidizi katika kuwarahisishia wanawake kuwasiliana kwenye mambo mbalimbali na kupata taarifa zinazoendelea ndani ya nchi.

Abeid amesema, Shirika lao lilifanya tafiti mwaka 2017 zilizohusisha kujifunza changamoto wanazopitia wanawake na wasichana wenye ulemavu hasa katika ukatili hapa nchini.

“Kutokana na ugonjwa uliokuwepo awali wa Corona tuliamua kuja na hizi simu ili kurahisisha katika mawasiliano hata kama wakiwa na vikao kuwasiliana moja kwa moja bila kuwa na muingiliano,”.

“Pia tunaamini kupitia mradi huu tutawafikia walemavu wengi zaidi kwani unatarajia kuisha mwaka 2022 tutaendelea kusaidia jamii ili kuwarahisishia kupata taarifa mbali mbali,”Amesema

Mwenyekiti wa wanawake na watoto wenye ulemavu Tanzania, Nuru Awadhi amelishukuru Shirika la Kimataifa la Add kwa Msaada waliowapatia utajkaoweza kuwasaidia katika mawasiliano.