September 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanasiasa chanzo cha ndoa za utotoni,ukeketaji Tarime

Na Penina Malundo,Timesmajira
SHRIKA linalopinga Ukeketaji la Terminationof Female Genital Mutilation(ATFGM) Wilayani Tarime Mkoani Mara limesema kuwa wanasiasa wanaonekana kuwa chanzo kikubwa cha uwepo wa ndoa za utotoni na ukeketaji kwa wilaya hiyo kwa kushindwa kuyaongea kwa jamii kwa lengo la kulinda nafasi zao.
Pia limesema kwa miaka ya uchaguzi mara nyingi kumekuwa na ongezeko la wahanga wengi wanaopitia masuala ya ukeketaji na ndoa za utotoni kutokana na wanasiasa kuyafumbia macho masuala hayo kwa kulinda kura zao.

Akizungumza jana mkoani humo wilayani Tarime ,Meneja Miradi wa ATFGM,Valerian Mgani wakati wa Mtandao wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni Tanzania (TECMN) walipofanya ziara katika Kituo chao kinachopokea wahanga wa ukeketaji na ndoa za utotoni kutoka maeneo mbalimbali ambapo wasichana hao ukimbilia mahali hapo kama sehemu ya kujiokoa na matukio hayo kutopata.

Mgani amesema wanasiasa kuyafumbia macho mambo hayo yanakuwa sababu yankuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa wilaya hiyo.

“Suala la siasa limekuwa ni changamoto wanasiasa karibu wote hakuna ambaye anaweza kusimama jukwaani na kuongea masuala haya yav kupinga ndoa za utotoni wala suala la ukeketaji,wanasiasa wengi huku wameshajichukulia wakitaka wachaguliwe na kuendelea kuwepo katika madaraka ni lazima yeye aweze kuwa upande wa wananchi hasa katika upande wa kutetea masuala ya ukeketaji na ndoa za utotoni.

“Kila mwaka wa uchaguzi kumekuwa na changamoto hii kuwa kubwa ,Mfano mwaka 2020 kumekuwa na changamoto kubwa ya idadi ya watoto kukimbilia katika kituo hicho kutokana na wengi kutaka kukeketwa na wengine kuozeshwa wakiwa na umri mdogo na hii inatokana na watu kuwa bize na masuala ya siasa na kushindwa kuwatetea watoto,”amesema.

Amesema kwa mwaka huu hali hiyo imeanza kuonekana mapema hivyo wao kama asasi na kituo wanategemea kupokea wahanga wa masuala ya ukeketaji na ndoa za utotoni zaidi ya watoto 700 kituoni hapo.

“Tumejipanga kuwapokea wahanga wa ukeketaji na hao watoto wanaoozeshwa kwa umri mdogo na pia tumejipanga kufatilia maeneo ambayo yameanza kufanya vitendo hivyo kwa ukaribu zaidi,”amesema.

Mgani amesema serikali inahitaji kuweka nguvu nyingine ya ziada hasa kwa wanasiasa kuwasaidia watoto hao wa kike wanaposimama majukwaani waweze kuongea masuala ya kupinga mambo ya ukeketaji na kupinga ndoa za utotoni.

Amesema wahanga namba moja ni katika matukio hayo ni wale watoto waliomaliza tayari darasa la saba na suala la biashara kwa wazee wa kimila na Ngariba kuwalazimisha watoto wakike kuolewa ili wao wapate fedha.

Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao huo,Lilian Kimati amesema lengo la Caravan hiyo ni kupita katika mikoa minne ambayo ina asilimia kubwa ya ndoa za utotoni ikiwemo mkoa wa Mara ,Shinyanga,Tabora pamoja na Dodoma.

“Mtandao wao ulianzishwa mwaka 2012 na kipindi hicho kulikuwa na changamoto kubwa ya ndoa za utotoni hivyo walijiunga kwa lengo la kuwa na sauti moja ili kutokomeza ndoa hizo za utotoni ambapo ulianzishwa na mashirika 12 ila kwa sasa mtandao unamashirika 87 ambayo unafanya kazi Tanzania nzima na Zanzibar,”amesema

Amesema lengo la caravan hiyo ni kupita katika mikoa ambayo inaasilimia kubwa ya ndoa za utotoni ambapo kwa sasa ni awamu ya pili lengo ni kuzungumza na wasichana na kuwapa elimu za masuala ya ndoa
za utotoni na jinsi gani wazazi wanatakiwa kusimama katika nafasi zao kuhakikisha mabinti hawaozeshwi mapemana kwenda shuleni ili kufanya mambo makubwa.

Amesema miongoni mwa mashirika ambayo yameongoza katika Caravan hiyo ni pamoja na wanachama wa Mtandao huo kutoka Shirika la Msichana Initiative,Binti Makini,Medea,Plan Internationa pamoja na My Legacy.