Na Mwandishi Wetu,Jeshi la Polisi.
KIKOSI cha wanariadha wa Tanzania kilicho fanya vyema katika mashindano ya Mbio ndefu na fupi katika michuano ya mbio maarufu NAGAI City Marathon 2023 kimepongezwa kwa kuiletea sifa nzuri Nchi yetu baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika mbio zote.
Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Dotto Mdoe kwa Niaba ya Mkuu wa Jeshi la polisi wakati akiongoza mapokezi ya wanariadha hao ambao wanatoka Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi waliowasili Nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (KIA) jana jioni.
Mbio hizo za hisani na uimarishaji wa mahusiano baina ya Japan na Tanzania kupitia Michezo zilifanyika jijini Nagai nchini Japan, Oktoba 15, 2023,huku watanzania wakipeperusha vyema Bendera ya Tanzania katika michuano hiyo ya kimataifa ambapo mataifa kadhaa yalishiriki.
ACP Dotto Mdoe amesema wachezaji hao kwa Umoja wao wameendelea kuwa wazalendo kwa kuipambania Tanzania katika medali za Michezo lakini pia kuitangaza Nchi yetu katika sekta ya utalii kupitia mashindano hayo kwa kufanya vyema kwenye nafasi za juu.
Ameendelea kusema kuwa Jeshi hilo kwa kushirikiana na wadau wengine wa michezo wakiwemo Chama cha Riadha Tanzania litaendelea na Mikakati yake ya kuendelea kuwanoa wanamichezo wengine kwa ajili ya kufanya vyema katika mashindano ya ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Kwa upande wake Katibu wa Shirikisho la Riadha Nchini Bwana Jackson Ndaweka amesema kuwa Wanamichezo hao walitoka katika timu mbili yaani Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi ambapo kwa upande wa Jeshi la wananchi wanariadha wake waliibuka washindi wa kwanza katika michuano ya mbio za masafa marefu ambazo ni kimometa 42 lakini kwa Jeshi la Polisi wanaridha wake waliibuka washindi wa kwanza katika mbio fupi yaani kilometa 21.
Katika mashindano hayo Mwanariadha Sara Ramadhan ametawazwa kuwa mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake Mbio za masafa yaani kilometa 42 ‘Full Marathon’ huku pia kwa wanaume Peter Sulle akishinda na kufuatiwa na Fabian Joseph.
Kwa upande wa Mbio fupi yaani kilometa 21 Watanzania pia walifanya vyema “Half Marathon’, ambako kwa Wanawake Transfora Musa alishinda nafasi ya kwanza na Kwa upande wa Wanaume, ilishuhudiwa Josephat Gisemo akiibuka mshindi wa kwanza na kufuatiwa na Paul Damian Makiya.
Naye Transfora Musa kwa niaba ya wanariadha wenzake amemshukuru Rais kwa juhudi kubwa ambazo anazionesha katika sekta ya michezo hali ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kupelekea mafanikio yao.
Takwimu inaendelea kuibeba Tanzania katika mishindano hayo ambapo mwaka 2022 Tanzania ilifanya vyema katika Mbio hizo kupitia Mwanariadha Alphonce Simbu pamoja na Fabian Jesephat. uyu
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM