Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
SERIKALI ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikisha mtoto kike anamaliza elimu ya msingi na sekondari , imetoa fursa ya kuendelea na masomo kwa wasichana ambao wanapata ujauzito wakiwa katika shule za msingi au sekondari .
Aidha ,wanafunzi hao wataruhusiwa kuendelea na masomo katika mfumo rasmi wa elimu baada ya kujifungua.
Vile vile imetoa nafasi kwa wanafuzi wa darasa la saba walioshindwa kumaliza darasa hilo kwa namna yoyote ile ,kufanya mtihani wa marudio mwaka unaofuata.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka 60 baada ya Uhuru katika sekta ya elimu nchini.
Profesa Ndalichako amesema,Serikali itatoa nafasi kwa wanafunzi hao kuendelea na masomo kutokana na takwimu kuonyesha kuwa watoto wanaacha shule kwa sababu mbalimbali.
“Takwimu za elimu zinaonyesha kwamba wanafunzi wanaacha shule kutokana na sababu mbalimbali ukiwemo utoro, ujauzito, utovu wa nidhamu,lakini sababu kubwa ni utoro ambapo wanafunzi wa shule za msingi ni takribani 108 ambapo asilimia takriban 93 ni watoro na asilimia 5 wanaacha shule.”amesema Profesa Ndalichako na kuongeza kuwa
“Lakini tumesema hata hawa asilimia tano wanaocha shule kwa sababu ya utoro pengine wanaweza kuwa na sababu ya msingi ya utoro wao,inawezekana kuna changamoto za kifamilia zikiwemo za kiuchumi ,kuuguliwa,kuhama maeneo
“Lakini serikali imesema yule atakayekamilisha kutatua changamoto zilizokuwa zikimkabili anaweza kurudi shule ndani ya miaka miwili tangu alipoacha shule.”
Akizungumzia kuhusu wanafunzi wa darasa la saba wanaoshindwa mtihani wa darasan hilo kwa sababu mbalimbali amesema,wanafunzi hao sasa wanapewa nafasi ya kurudia mitihani yao kwani huenda waliacha shule kwa sababu za msingi.
“Kwa waliomaliza darasa la saba na kushindwa mtihani kwa namna yoyote ile ikiwemo kufutiwa matokeo ,wataruhusiwa kufanya mtihani wa marudio .”
Profesa Ndalichako amesema, utaratibu wa wananfunzi hao kurudia mtihani utawekwa na baraza la mitihani huku akisema, wanafunzi watakaorudia mtihani ambao watafaulu mtihani huo watapata fursa ya kuchaguliwa katika shule mbalimbali hapa nchini kujiunga na shule za sekondari.
Hatua hiyo ni kuzingatia kwamba wanafuniz wa kidato cha nne na sita wanapata fursa kwa hiyo serikali imeona iwapatie fursa na wananfiunzi wa darasa la saba am,bao bado ni wadogo.
Ametoa wito kwa wasimamizi wa mitihani wazitingatie sharia,taratibu na miongozo iliyowekwa kwani serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa wale wote watakaojihusisha na wizi wa mitihani kwa namna moja ama nyingine.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa