
Na Mwandishi Wetu, Mbozi
MUSA Kayala, mkazi wa Mtaa wa Namlea, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe, amenusurika kuuawa na wananchi wenzake, huku nyumba yake ikinusurika kuchomwa moto baada ya kutuhumiwa kuhusika na uhalifu na vitendo vya ukatili dhidi ya familia yake.
Tukio hilo limetokea Septemba 5, 2026, majira ya saa 8:00 Alfajiri, baada ya Kayala kudaiwa kuingia kwenye nyumba ya mwananchi kwa lengo la kuiba pikipiki, lakini hakufanikiwa na kukamatwa.
Baada ya kukamatwa, wananchi walidaiwa kumshushia kipigo kikali kabla ya uongozi wa mtaa kuingilia kati na kumuwekq chini ya ulinzi kisha kutoa taarifa polisi.

Hata hivyo, wakati polisi wakifika eneo la tukio tayari walikuta wananchi wametoa vyombo vyotenje tayari kuichoma nyumba moto.
Wananchi hao walitishia kuichoma nyumba yake moto, lakini viongozi wa Mtaa wakiongozwa na Mwenyekiti Elesea Mgandilwa waliingilia kati na kuzuia tukio hilo.
Jeshi la Polisi lilifika eneo hilo majira ya saa 3:20 asubuhi na kumchukua Kayala kwa ajili ya uchunguzi na hatua za kisheria.

Baadhi ya wananchi walidai Kayala amekuwa akihusishwa na matukio mengine, yakiwamo madai ya kuwamchoma mtoto na mke wake kwa kisu, na kumfanyia ukatili wa kingono mbele ya watoto wake, pamoja na wizi na vitisho.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Mtaa huo hakuwa tayari kueleza kwa kina tukio hilo pamoja na tuhuma hizo kwa kuwa aliondoka na polisi kwenda kituoni.
Baadhi ya wananchi wakiwa mbele ya kiongozi wa polisi, aliyejitambulisha kwa jina moja la Afande Simion, aliwaasa wananchi kutojichukulia sheria mkononi.

Kauli ambayo ilipingwa wazi na wananchi hao na kusema hawataki Kayala kurejea eneo hilo, wakihofia usalama, huku viongozi wakisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia vyombo vya sheria badala ya kujichukulia hatua.


More Stories
EACOP kukamilika Januari 2027
TMA yatakiwa kuimarisha utabiri wa hali ya hewa
Haule aungana na wananchi kuchimba msingi wa shule