January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanandoa washikiliwa kwa tuhuma za mauaji Kagera

Na Ashura Jumapili,timesmajira,Bukoba


JESHI la polisi Mkoani Kagera linawashikilia wanandoa wawili   kwa tuhuma za mauaji ya kikongwe wa miaka  ( 71 ) Wilayani Missenyi Mkoani humo.

Kamanda wa polisi Mkoani humo.Jumaa Awadhi,amethibitisha kutokea kwa tukio wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Jana ( leo ) amewataja wanandoa hao kuwa ni Robert Berenando raia wa Burundi  miaka ( 19 ) Mkulima na mkewe Benadetha Robert Msubi miaka ( 19 ) Mkulima.


Amesema watuhumiwa hao walihusika na tukio hilo la mauaji Octoba 15,mwaka huu Majira ya saa tisa na nusu alasiri Kijiji cha Buharata Wilayani Missenyi  walimuua Theopista Laurent miaka ( 71 ) mkazi wa Kijiji hicho cha Buharata.


Amesema watuhumiwa hao baada kufanya tukio hilo la mauaji walitoweka na kwenda kusikojulikana.


Amesema polisi baada ya kufanya uchunguzi  walifanikiwa kuwakamata Octoba 31 mwaka huu Majira ya saa mbili usiku Kijiji cha Kiluluma tarafa ya Nyabiyonza Wilayani Karagwe.


Kamanda Awadhi amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa wanandoa hao walikuwa wafanyakazi wa marehemu walikuwa wakifanya shughuli za kilimo na kuwa walikuwa hawalipwi ujira wao kwa muda mrefu.


Amesema Jeshi la polisi likikamilisha uchunguzi wake watafikishwa mahakamani.

Wakati huohuo Jeshi la polisi linawashikilia watuhumiwa wawili  kwa kosa la kupatikana na Nyara za serikali huku akiwataja watuhumiwa hao kuwa ni Tawabu Almas miaka ( 35 ) mhaya mkazi wa Minziro Wilayani Missenyi na Joseph Kagwa ( 42 ) mhaya mkazi wa Minziro.


Amesema Novemba 6,mwaka huu  Majira ya saa tano asubuhi  maeneo ya  Nyakahanga Kijiji cha Minziro  Wilayani Missenyi Askari waliokuwa katika Doria  walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na mfupa wa mguu wa Tembo  na meno ( Magego ).