Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dodoma
WANANCHI waendelea kupatiwa msaada mbalimbali wa kisheria kupitia, kampeni ya Mama Samia Legal Aid Kampen iliyopo chini ya Wizara ya Sheria na Katiba.
Kupitia kampeni hiyo watalamu wamepiga kambi katika maonesho ya Nanenene jijini Dodoma yanayofanyika viwanja vya Nzuguni na kupatika msaada wa kisheria.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, wananchi walimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada huo, huku wakishauri utaratibu huo uwe kitaasisi ili uweze kudumu kwani unasaidia wananchi kupata haki zao na kumaliza migogoro ya kisheria.
Mkazi wa Manisipa ya Dodoma Kata Nzunguni, Luciana Mwanitu, alisema kwamba aliamua kufika kwenye banda hilo ili aweze kijifunza kazi zao wanazozifanya za kutoa huduma kwa wananchi.
“Nimeelimishwa kuhusu Mpango wa Mama Samia, lakini nashauri jambo moja hii ni taasisi mpya na watu wengi hawafahamu kuhusu hii taasisi na kazi yake, kwaiyo ni muhimu sana kuongeza elimu hii katika maeneo mbalimbali ya nchi hasa maeneo ya vijijini,” alisema.
Aidha, alimpozega Rais Samia kwa kutoa huduma ya elimu kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aid, kwani huduma hiyo ni muhimu sana kwa wananchi kwa sababu wapo watu wengi wanashindwa kupata haki zao kwa kukosa msaada wa kisheria.
Mwananchi mwingine, Renatha Manda, alisema ametembelea banda hilo la sheria la Mama Samia na amekutana na maofisa wamempatia msaada wa kisheria.
“Nashukuru sana nilikuwa tatizo la kisheria, lakini nimekuja hapa nimepatia msaada wa kisheria na tatizo limeisha, ” alisema.
Pia nimepatiea ushauri na elimu nzuri kuhusu masuala ya kisheria na najipanga vizuri kwenye kuweka mirathi.” Alisema mpango huo ni mzuri kwa kuwasaidia wananchi wasio na uwezo ambao hawana uwezo wa kuweka Mawakili.
Mkazi wa Shinyanga Mjini, Uwezo Maulid,alisema alimua kufika kwenye Maonesho ya Nane nane ili asaidiwe kupate haki ya mirathi ya mume wake.
“Mume wangu alikuwa mtumishi wa umma katika Manispaa ya Shinyanga, nilienda mahakamani ili wanagu na mimi mwenyewe tupate haki kuhusu mali za maremu, lakini sitendewi haki huu ni mwaka wa nne tangu marehemu afariki, lakini mpaka dakika hii sijapata hata shilingi mia alizoacha marehemu mume wangu na katika nyumba tuliyokuwa tunaishi nimefukuzwa na baba wa marehemu,”alimesa.
“Nimekuja hapa ili nisaidiwe,mimi na wanagu tupate msaada wa kisheria na ninaamini nitasaidiwa.”
More Stories
Bodaboda wamchangia Rais Samia Mil 1 ya fomu ya Urais
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani