May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi wavutiwa na utalii Ikolojia

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Wananchi mbalimbali wameendelea kutembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii hususani eneo la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambapo wamekuwa wakipata elimu kuhusu uhifadhi wa misitu na mazingira na ufugaji wa nyuki

Hata hivyo Utalii Ikolojia umekuwa ni kivutio kikubwa kwa wananchi wanaotembelea maonesho haya ya Sabasaba ambapo kutokana na uhifadhi wa misitu unapelekea wananchi kupata maeneo mazuri ya kupumzika ambayo ni tofauti na mboga za wanyama zenye wanyama wakali.

Akizungumza Meneja wa Mipango na Masoko – TFS, Neema Mbise amesema kuwa Wakala inaendelea kutoa elimu kwa wananchi katika Maonesho haya ya Sabasaba kuhusu uhifadhi , biashara ya mazao ya misitu na masuala ya Utalii Ikolojia ambapo wakifika watakutana na ofa mbalimbali za kutembelea maeneo ya vivutio katika Hifadhi za misitu.

“Wakifika hapa watakuta wataalamu ambao watawapa elimu mbalimbali kuanzia upatikanaji wa mbegu bora za miti mbalimbali, duka la asali ambapo watapata elimu na bidhaa zitokanazo na mdudu nyuki.”

“Lakini tumewaletea bustani hapahapa sabasaba na bila kusahau tuna Shamba la nyuki ambapo wanapata Utalii wa nyuki kea kuona maisha ya mdudu nyuki kwa ujaribu na faida zake kimazingira na kiuchumi hivyo tunawakaribisha sana” Amesema Neema Mbise.

Wananchi wamefurahia uwepo wa maeneo hayo mengi ambayo yanawawaweka karibu na viumbe mbalimbali ambavyo wanaweza kujifunza maisha ya wanyama na wadudu mbalimbali kwa ujaribu zaidi.

Ukitembelea banda la Maliasili na Utalii sehemi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania utaweza kuona namna upandaji miti, uhifadhi wa misitu, ufugaji nyuki na Utalii Ikolojia unavyofanyika.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi ambao wametembele eneo la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika Maonesho haya ya DTIF ( Sabasaba) wameipongeza TFS kwa kuwapa elimu ya utunzaji misitu na mazingira kwa ujumla.

” Ni wajibu wetu kutunza mazingira hususani misitu yetu kwani inatusaidia katika maisha yetu ya kila siku, kwa kweli nimefurahi sana kwa elimu niliyoipata hapa nitakuwa balozi mzuri”

Athumani Majidi amesemaHata hivyo wameendelea kusisitiza elimu ya utunzaji mazingira iendelee kutolewa ili kusaidia wananchi wengi zaidi katika kupanda miti na kuendelea kutunza mazingira kwani inapelekea uwepo wa maeneo mazuri ambayo wamekuwa wakiyatembelea.

” Tumekuwa tukitembelea mbuga za wanyama lakini hili ya Utalii Ikolojia ni zuri zaidi kwani maeneo haya unaweza kutembea vizuri msituni kwa miguu na kujionea ndege wadudu na wanyama mbalimbali ambao sio wakali, kwa kweli ukiwa mle lazima akili itulie sababu kunakuwa kumetulia sana na hewa ni safi zaidi”.

Joyce Anthony AliongezeaWakala wa Huduma za Misitu Tanzania wapo Viwanja vya Sabasaba hadi tarehe 13 Julai 2023 kwaajili ya kuonesha fursa mbalimbali zinazopatikana katika misitu na wanawakaribisha wananchi kutembelea katika maeneo yenye vivutio vinavyopatikana katika Hifadhi za Mazingira Asilia na kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza katika fursa mbalimbali zinazopatikana katika misitu hiyo.