January 27, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi waombwa kumuunga mkono dkt Tulia

Na Esther Macha , Tmesmajira,Online, Mbeya

Wananchi na wadau mkoani Mbeya wameombwa kumuunga mkono Spika wa Bunge,Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson kwa kuhakikisha mbio za Tulia Marathon zinakuwa endelevu,kutokana na fedha zinazopatikana kwenye mbio hizo kuchochea sekta ya elimu na afya.

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, SumaFyandomo wakati akizungumza na Timesmajira online mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini hapa.

Fyandomo amesema kuwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya waendelee kuwa na moyo wa kujitokeza kwa wingi kila mwaka yanapofanyikamashindano ya Tulia Marathon kwani fedha ambazo zikipatikana zimekuwa zikisaidia kuboresha elimu na afya .

‘’Toka kuanza Mashindano mimi nimeshiriki mara saba,nawaomba ndugu zangu tujitokeze kwa wingi ili kuunga mkono kwa jambokubwa ambalo amekuwa akifanya kila mwaka kwa kuzingatia kuwa michezo ni afya”,amesema.

Amesema kuwa kupitia mashindano hayo pia yamekuwa yakitoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wazawa na kutoka nje ya Mkoa wa Mbeya hivyo kama Wabunge wana kila sababu ya kuunga mkono.

Kwa upande wake Diwani wa Viti Maalum Kata ya Isanga Atu Msayi amesema kuwa Tulia Marathon imekuwa ikileta fursa za kiuchumi kwa wajasiliamali mbalimbali katika Mkoa wa Mbeya

.‘’Kikubwa wana Mbeya tuendelee kumuunga mkono Spika na Mbunge wa jimbola Mbeya kila anapofanya Tulia Marathon iwe ndani na hata nje ya Mbeya ili kuweza kuendelea kuboresha sekta ya elimu.