Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Mara
KATIKA hali isiyotarajiwa wananchi wa kijiji cha Nkerege kata ya Kiore wilayani Tarime Mkoa wa Mara, wameamua kushirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya katika zoezi la kufyeka na kuteketeza mashamba ya bangi ili kuleta hali ya amani na utulivu kijijini hapo.
Uamuzi huo umetokana na hofu iliyojitokeza wakati wa operesheni ya kuondoa bangi, ambapo watu walikimbia makazi yao wakihofia kukamatwa jambo lililoathiri shughuli zao za kijamii na kiuchumi.
Akizungummzia sakata hilo , Diwani wa Kata ya Kiore, Rhobi John, ameeleza kwamba, wananchi wa Nkerege kwa kauli moja,wamesema wameikataa bangi na kilimo hicho na kwamba, hakitalimwa tena kijijini hapo.
“Jana usiku wakina baba, wakina mama na vijana wote wameamua bangi haitaonekana tena, yaani sisi wenyewe tutakuwa walinzi sisi kwa sisi, unapoona mwenzako analima ni lazima kufuatilia na kutoa taarifa. Naishukuru cabinet ya wanasheria kutoka Mamlaka kutoa elimu, akina mama na vijana waliikuwa hawajapata elimu na walidhani hili ni zao bora kwao”amesema John.
Mzee Julius ZakariMatiku, mwenyekiti wa mila katika ukoo wa Wasweta, alisema, “Tumekubaliana kuteketeza bangi ili kuondoa tatizo hili la kukimbiakimbia, Kijana atakayekamatwa akilima bangi, nitalipiza faini ya ng’ombe watano. Mzee wa mila ana jukumu la kuhakikisha kuwa sheria zinaheshimiwa katika kijiji.
Kadhalika, Katibu wa Mila Burima Nyawise amesema, wao kama wazee wameamua kuteteketeza bangi ili waweze kulima mazao mengine kama mahindi, ufuta na kuendelea kufuga mifugo yao katika pori hilo. ” Pori hili ni safi kwa kulima kitu chochote kama vile mahindi maharage ufuta vinakubali, kwa hiyo, hili zao la bangi limetutosha. Sasa watoto watulie nyumbani, wanawake wapikie watoto na sisi malengo yetu ya kuja humu ni kuhakikisha tumeliteketeza hili zao la bangi” amesema.
Mamlaka ya Kudhiitia Kupambana na Dawa za Kulevya inaendelea kufanya operesheni nchi nzima ili kuhakiksha dawa za kulevya za mashambani na viwandani zinatokomea na Tanzania inakuwa huru dhidi ya dawa za kulevya. Hivyo, ni jukumu la kila mmoja kupiga vita dawa za kulevya. Tusikubali kuwa sehemu ya kuangamiza taifa letu kwa kuendelea kulima na kufanya biashara ya dawa za kulevya
More Stories
NIDA yawakumbusha wananchi kuchukua vitambulisho vyao
Dkt.Kafumu:Uteuzi wa Rais Samia umezingatia katiba
Kliniki ya sheria bila malipo yazinduliwa Kilimanjaro