November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi waitwa kutembelea kijiji cha Bima

Na Joyce Kasiki Timesmajira online

MSULUHISHI wa Migogoro ya Bima kutoka wakala wa Usimamizi wa Bima (TIRA)  Margaret Mngumi amewaasa wananchi kutembea banda la kijiji cha Bima ili wapate elimu ya bima itakayowawezesha kujiunga na bima mbalimbali na hivyo kujikinga na majanga.

 Mngumi ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Kijiji cha Bima kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara  (Sabasaba) .

Amesema wao kama Bima wanatumia maonesho hayo kuhudumia wateja wanaofika katika banda lao wenye changamoto za bima.

“Tunatumia maonesho haya kutoa elimu lakini pia na kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi ikiwemo migogoro ya bima,kwa hiyo tunawakaribisha wananchi katika banda  letu wanapata elimu ya kutosha kuhusu bima.”amesema Mngumi

Mwakilishi wa Kampuni za Bima zinazoshiriki maonesho ya Sabasaba, Alilya Kwayu kutoka kampuni ya Bima ya BUMACO amewaasa watanzania kukata bima kwa ajili ya maisha yao.

“Bima ni maisha ,ukijata bima unakuwa na uhakika wa unachokimiliki,kwa hiyo nawaasa wananchi wenzangu wakati bima ili kujikinga dhidi ya majanga mbalimbali.”amesema Kwayu

Naye Meneja Uandikishaji kutoka Kampuni ya Bima Mtawanyo  Charles Chanya, amesema wao wanashughulika na kutoa huduma kwa makampuni ya bima kwa lengo la kuyaongezea uwezo katika shughuli zao za kila siku.