January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi wahimizwa kuunganishanguvu kutokomeza ukatili kijinsia

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online,Ileje

WANANCHI wilayani Ileje mkoani Songwe, wameshauriwa kuungana, na kushirikiana kwa pamoja ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi, wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kipinga ukatili wa kijinsia wilayani hapa.

Akizungumza wakati alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, Mgomi alitoa wito kwa wananchi kubadilika na kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Amewataka wananchi kukemea na kushirikiana na vyombo vya dola kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, ili kuhakikisha jamii inabaki salama dhidi ya vitendo hivyo.

“Vitendo hivyo vinarudisha nyuma ustawi wa jamii na kuzorotesha uchumi wa Taifa kwa ujumla,” alisema.

Aidha, amewataka wazazi kuwalinda watoto kwa kuwapa malezi stahiki yanayozingatia maadili ya Kitanzania, ili kuwaepusha watoto kuiga tamaduni za nje, ambazo zinakiuka miiko ya maadili ya nchi.

Wakati huo huo, DC Mgomi ameshauri familia kudumisha upendo na kuepuka migogoro na kutumia fursa zilizopo katika wilaya hiyo ili kujiongezea kipato kitakachowasaidia kutunza na kulea familia.

Mwishooooooooooooooooo