November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi wahimizwa kuachana na kilimo cha bangi,mirungi

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

KAMISHNA Msaidizi wa Kinga na Huduma za Jamii katika Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya nchini (DCEA) , Moza Makumbuli amesema,Mamlaka hiyo imeshiriki maonesho ya wakulima na wafugaji (88) ili kuwaelimisha wananchi waweze kuachana na kilimo cha bangi,mirungi lakini pia kuachana na matumizi ya dawa za kulevya kwa ujumla.

Akizungumza kwenye banda la Mamlaka hiyo iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu,Makumbuli amesema ,wananchi wengi wamekuwa wakijishughulisha na kilimo haramu cha bangi na mirungi mazao ambayo yanawaathiri vijana ambao ndiyo nguvukazi ya Taifa.
Amesema katika maonesho hayo mamlaka hiyo inahusika kwa kuwa kuna baadhi ya dawa za kulevya zinatokana na kilimo haramu zinazolimwa hapa nchini zikiwemo bangi na mirungi.

“Tumekuja na mbangi wenyewe. Tunapinga kilimo cha bangi. Hivyo tumeleta sampuli za dawa mbalimbali za kulevya ili watu wazitambue na kutoa taarifa,” amesema.

Amesema kwa Tanzania bangi inalimwa katika maeneo mengi, inapelekwa mpaka nje ya nchi, na kutaja maeneo yanayoongoza kwa kilimo hicho kuwa ni Mara, Arusha, Tabora na Pwani.

“Same mkoani Kilimanjaro ni makao makuu ya kuzalisha mirungi. Nasi hatutachoka kuelimisha wananchi kuwa kilimo hicho ni haramu.”

Ametumia nafasi hiyo kuwasihi wananchi hasa wakulima wafike kwenye banda hilo ili wapate elimu kuhusu biashara haramu ya dawa za kulevya.

“Mbali na bangi na mirungi ,pia tupo kwa ajilo ya kutoa elimu kuhusu matumizi haramu ya dawa nyingine za kulevya kama vilw cocain na heroin,tunaielimisha jamii kuachana na matumizi hayo kwani siyo salama kwa afya zao.”amesema Makumbuli