January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi wahimizwa kushiriki mazoezi

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela Said Kitinga,amesema ni muhimu kwa wananchi kufanya mazoezi ili kuondokana na magonjwa nyemelezi na kuisaidia serikali katika kupambana na maradhi.

Hayo ameyasema mara baada ya kumalizika kwa mbio za Ilemela Jogging Club ambazo zimeandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla zinazofanyika kila Jumamosi ya wiki ya pili ya kila mwezi.

Ambapo mbio hizo za Kilomita 16 kutoka uwanja wa CCM Kirumba kupitia Pasiansi kuelekea Ilemela Redio Free na kisha kurudi CCM Kirumba zilishirikisha vilabu vya mbio vinavyopatikana katka Mkoa wa Mwanza ikiwemo Wasafi Jogging, EFM Jogging, Isamilo jogging, Rock City Runners, Samia Jogging na Ilemela Watumishi Jogging

Kitinga,amesema ni muhimu kwa wananchi kufanya mazoezi ili kuondokana na magonjwa nyemelezi na kuisaidia serikali katika kupambana na maradhi pamoja na kuimarisha afya.

Pia amesema mazoezi yamekuwa chachu katika kuleta umoja, upendo na mshikamano hivyo wananchi wajitokeze katika kufanya mazoezi.

Kaimu Ofisa Michezo wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Kizito Bahati Akizungumzia namna wanavyitekeleza agizo la Waziri Mkuu kwa vitendo kuhusiana na wananchi kuhamasishwa kushiriki mazoezi.

“Mbio hizi ni utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hivi karibuni wakati wa kikao chake na Maofisa Michezo wote nchini cha kutaka kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi ambapo Ilemela tulikuwa tumeisha anza chini ya Mkuu wetu wa Wilaya,”amesema.

Mmoja wa washiriki wa mbio hizo,amewahimiza wananchi wenzake kuendelea kuiunga mkono Serikali katika shughuli mbalimbali za kijamii inayozianzisha ikiwemo michezo na kushiriki mazoezi ili kupinga na adui maradhi.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela Said Kitinga,akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mbio za Ilemela Jogging Club ambazo zimeandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla zinazofanyika kila Jumamosi ya wiki ya pili ya kila mwezi. (Picha na Judith Ferdinand)
Kaimu Ofisa Michezo wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Kizito Bahati,akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mbio za Ilemela Jogging Club ambazo zimeandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla zinazofanyika kila Jumamosi ya wiki ya pili ya kila mwezi. (Picha na Judith Ferdinand)
Baadhi ya washiriki wa mbio za Ilemela Jogging Club ambazo zimeandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla zinazofanyika kila Jumamosi ya wiki ya pili ya kila mwezi.(Picha na Judith Ferdinand)