November 12, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi Visiwani Zanzibar kunufaika na Nishati jadidifu

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

WIZARA ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar imekusudia kuwanufaisha wananchi visiwani humo katika kutumia nishati Jadidifu kutokana na kuwa rafiki.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam wakati wa kuhitimisha jukwaa lililowakutanisha wadau wa Nishati mbadala, Katibu mkuu wizara ya Maji, Nishati na Madini visiwani humo Dkt Mngereza Miraji amesema kwa kuanzia tayari serikali imeanza utekelezaji wa mradi uliyofadhiliwa na Benki ya Dunia ili kufikisha huduma hiyo.;

“Utekelezaji wa miradi huu wa World Bank umeshaanza ambapo ulianza Desemba 2021 na sasa hivi tayari wajenzi na wakandarasi wanaendelea na kazi Zanzibar”

Amesema kaya zaidi ya 140 imenufaika na huduma hiyo katika visiwa vya Kokota na Njau huku megawati 18 unatarajia kuwanufaisha kaya zaidi ya laki tatu.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo Katibu tawala mkoa wa Pwani Mwanaasha Tumbo amesema vifaa hivyo vimeghalimu shilingi milioni 600 huku utekekelezaji wake utafanyika katika wilaya ya Kibiti na Mafia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Water Kiosk Mhandisi Samuel Kinyanjui amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza matumizi ya maji chumvi katika maeneo hayo.

Jukwaa hilo limewakutanisha wadau mbalimbali ili kujadili changamoto na fursa zilizopo katika sekta ya nishati jadidifu ambalo limeanza juni 28 hadi 30.