Judith Ferdinand, Timesmajira Online,Mwanza
Wananchi wa mtaa wa Nyamanoro Mashariki na Mkudi Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela mkoani Mwanza,wametimiza msemo wa iwe mvua au jua lazima kazi iendeelee,baada ya kuendelea kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaofanyika nchi nzima Leo Novemba 27,mwaka huu, Jolicha ya kunyesha kwa mvua,maeneo mbalimbali mkoani humo.
Wakizungumza Novemba 27,2024, Timesmajira Online, wilayani Ilemela, baadhi ya wananchi hao waliojitokeza kupiga kura katika maeneo hayo,akiwemo Mkazi wa Nyamanoro Mashariki Tobiath Mbonde,amesema ameshiriki kupiga kura na zoezi limeenda vizuri ingawa kunachangamoto ya mvua kunyesha.
“Licha ya majina yetu yaliobandikwa nje ya kituo cha kupigia kura kulowana na mvua na kushindwa kusomeka,haijatuzuia kupiga kura kwani,wasimamizi katika vituo vya kupigia kura walitutaka tuingie ndani kisha tunataja majina yetu wanatuangalizia kwenye daftari kisha wanatupa karatasi na kiendelea na zoezi la upigaji kura,ambazo zoezi limeenda vyema kwa amani na usalama mpaka sasa,”.
Huku akisema matarajio yake,ni kupata viongozi watakaowatumikia wananchi kwani nao wametimiza wajibu wa kuwachagua bila ya vurugu.
Kwa upande wake Elizabeth Kalonga,kutoka mtaa wa Nyamanoro Mashariki,amesema ametimiza haki yake ya msingi kupiga kura mapema,na zoezi limeenda vizuri.
“Hali ya kupiga kura zoezi limeenda vizuri,ingawa mvua imekuwa nyingi,tunatazamia kwa sasa hali ya hewa imekuwa nzuri naimani watu watajitokeza kwa wingi zaidi,maana hata kwenye mvua watu wamejitokeza,”.
Mgombea nafasi ya Uenyekiti mtaa wa Nyamanoro Mashariki kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),Uswege Mwakalindile,utaratibu wa uchaguzi umeenda vizuri ingawa mashaka tulionayo ni majina yaliobandikwa nje ya kituo hayasomeki.
“Kama zoezi litaendelea kama sasa,na baadae lisitokee lolote uchaguzi utakuwa salama,ingawa kuna taarifa kuwa kuna maboksi ya kura kwa upande wa wenyeviti ikitokea hiyo itavuruga uchaguzi,vinginevyo mpaka sasa uchaguzi upo vizuri,”.
Amesema licha ya mvua kunyesha lakini hali ya wananchi kujitokeza kupiga kura katika eneo hilo ni nzuri,na anaimani hata shinda katika uchaguzi huo.
“Nikishindwa kwa haki sina neon,lakini nikishindwa kwa kuibiwa kura kwa sababu nimegombea kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na siyo kutafuta kazi kwa ajili ya kulisha familia,sitaweza kufanya vurugu bali nitawaachia wananchi wenyewe waamue,”.
Naye Mgombea nafasi ya Uenyekiti mtaa wa Mkudi Kata ya Nyamanoro kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),Salum Heri,amesema,zoezi la kupiga kura limeenda vizuri,watu wa mtaa huo wamejitokeza licha ya mvua kunyesha.
“Zoezi la uchaguzi ni la wazi na haki,tunaamini matokeo yatakuwa mazuri hakutakwa na changamoto yoyote,watu wanakuja wanaona majina yao wanapiga kura.Ikitokea nimeshinda nitaendelea kutekeleza miradi mikakati ambayo tulikuwa tumeianza ambayo hatujaimaliza kwa sababu mimi natetea nafasi yangu ya uenyekiti,kama nitatokea wananchi wasiponipa kura za ushindi hiyo ndio demokrasia nitakubaliana nao na tutaendelea na maisha mengine,”.
More Stories
RC Mrindoko:Ufyekaji wa mahindi Tanganyika si maelekezo ya serikali
Walimu S/ Sekondari Ilala wafundwa juu ya maadili ya wanafunzi
Dkt. Samia afungua skuli ya sekondari Misufini, Bumbwini