January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi mtaa wa Zingiziwa Chanika watakiwa kupeleka kero zao ofisini

Na David Johntimesmajiraonline

UONGOZI wa Serikali ya Mtaa wa Zingiziwa wilayani Ilala Mkoa wa Dar es Salaam umewataka wananchi hususani wanaomiliki ardhi kuacha kulalamika kuhusu migogoro ya ardhi badala yake kufika katika ofisi za mtaa ili kutatua changamoto zao.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi hivi karibuni katika ofisi za serikali ya mtaa huo Ally Mkwanda Amesema kuwa anashangaa kuona wananchi wanalalamika kuhusu migogoro ardhi na mwisho wasiku kulaumu viongozi badala ya kufika ofisini.

Amesema kuwa ofisi ya serikali ya mtaa ipo kwa ajili ya wananchi hivyo nivema wakafika ofisini ili uongozi ushughulikie changamoto hizo lakini pia lipo baraza la nyumba la ardhi ngazi ya kata hiyo ndio kazi yao.

“Binafsi niwaomba wananchi hususani wanaomiliki ardhi kwenye Mtaa wangu waache kutoa Lawama nje huko kwani hata wanapouziana maeneo huko hawashirikishi serikali lakini wakishatofautiana ndio wanakuja. “Amesema mkwanda

Nakuongeza kuwa “Nivema kuja ofisi ya serikali kuja kujiridhisha na eneo ambalo unauziwa Kama nisahihi na halina mgogoro. Kufanya hivi itakuwa umeepusha malumbano na migogoro isiyolazima. “amesisitiza

Pia ameongeza kuwa pindi wanapokuja serikali ya mtaa wanapata fursa ya kupata muongozo wa kuelekezwa baraza la nyumba la kata ili changamoto yao iweze kufanyiziwa kazi huko.

Mkwanda Akizungumzia maendeleo ya mtaa ikiwa pamoja na suala la usalama wa mtaa amefafanua kuwa mtaa uko vizuri hakuna shida na wananchi wanaendelea kuchapa kazi lakini kubwa zaidi anaishukuru serikali kwa kazi inayofanya.

Amesema katika mtaa wake serikali imefanya kazi kubwa kwani serikali yao ya mtaa nimiongoni mwa serikali ambayo imefaidika na fedha mbalimbali kwaajili ya utekelezaji wa miradi mingi ikiwamo mikubwa na midogo.