March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi Mlele wahaidiwa neema CCM ikishinda

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online.

MGOMBEA Mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewaahidi wananchi wa Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi,neema ya kupelekewa miradi ya maendeleo endapo chama hicho kiashinda katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Balozi Nchimbi ameyasema hayo mapema lSeptemba 10, 2025,wakati akizungumza na wananchi wa Mlele, kwenye mkutano uliofanyika uwanja wa Chamanzi, Kata ya Inyonga.Ambapo amesema chama hicho kinadhamira ya kuendelea kuwaletea wananchi ikiwemo wa wilaya hiyo .

Ambapo vitajengwa vituo viwili vya afya na zahanati tatu huku upande wa elimu, chama hicho kimeahidi kujenga shule za sekondari 11 na madarasa 98 pamoja na kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa kuwapelekea miradi mipya ya maji itakayotekelezwa katika maeneo 16.

“CCM ni chama kilichojidhatiti kuwatumikia wananchi ikiwemo wananchi wa Wilaya hii.Yapo maendeleo mengi yamefanyika katika Wilaya hii kwa upande wa elimu, afya, miundombinu ya barabara na kilimo,”amesema Balozi Nchimi.

Katika upande wa miundombinu ya barabara, amesema, Serikali chini ya CCM itaenda kuboresha baadhi ya barabara ikiwemo kilomita 10 kwa kiwango cha lami kilometa 71 kwa kiwango cha changarawe katika Wilaya hiyo.

“Tukiangalia katika upande wa miundombinu ya barabara zetu kwa kiasi kikubwa maeneo mengi yanapitika vizuri, lakini katika miaka mitano ijayo tutaenda kuziboresha baadhi ya barabara,”.

Baada ya kuwasalimia Wananchi wa Nsimbo, Dkt. Nchimbi aliwanadi wagombea Ubunge wa majimbo mbalimbali ya Mkoa huo, akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Nsimbo, Anna Lupembe pamoja na Madiwani.

Aidha amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais kupitia CCM,Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025