Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto, amewataka wananchi wa Majohe kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura Julai mwaka Julai mwaka huu ili kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Meya Kumbilamoto alisema hayo Kata ya Majohe wakati wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya kata Majohe Diwani PASCHAL LINYAMALA alipokuwa akiwasilisha utekelezaji wa Ilani ya kata hiyo kuanzia kipindi cha January 2023 mpaka 2024 ,MEYA Kumbilamoto alimwakirisha Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Said Sidde.
“Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Majohe tunaelekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 hivyo akuna budi kila mmoja wetu kujiandikisha sehemu yake ya kupigia kura na tuwamasishe watoto wetu waliofikia umri wa miaka 18 waweze kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura ili waweze kupiga kura “alisema Kumbilamoto.
Aliwataka viongozi wa chama na Serikali Majohe kushirikiana pamoja katika kuleta maendeleo ya chama na Serikali katika kuunga mkono Juhudi za Dkt.Samia Suluhu Hassan.
WAKATI HUO HUO Meya Kumbilamoto aliwataka Majohe wawe wamoja wasigawanyike katika kipindi hichi chama chetu kinaelekea katika uchaguzi wa Serikali wala kuchafuana kwani kila mmoja ana haki ya kugombea na kuchaguliwa .
Aidha alisema Chama cha Mapinduzi CCM kikisema huyu ana faa Uchaguzi wa Serikali za mitaa kila mmoja anatakiwa kumuunga mkono na viongozi wa kata ,wilaya na mkoa itamuunga mkono kupeperusha Bendera ya CCM.
Akizungumzia Mafanikio na Maendeleo ya kata ya Majohe alisema Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan imetekeleza kwa vitendo imetoa zaidi ya shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kituo cha afya Majohe ambapo kwa sasa kinatoa huduma za mama na mtoto pamoja na huduma za Upasuaji wananchi wanapata huduma za afya ndani ya kata hiyo hawasumbuki kwenda mbali.
Alisema kwa sasa Majohe ina watu zaidi ya 1500,000 ambapo Serikali inaitazama kwa karibu ikiwemo kuwekeza huduma.za jamii .
“Mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji DMDP Dar es Salaam imepata barabara za kilometa 46 zikiwemo barabara za majohe zipo katika mradi wa DMDP na TENDA ya Barabara Serikali inatarajia kutangaza Juni 30 mwaka huu hivyo wananchi aliwaomba ushirikiano katika mradi huo wa DMDP .
Aliwataka wananchi wa Majohe kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa katika sekta ya afya na sekta ya Elimu .
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba