January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi Lukobe, Dkt.Angeline wapongezwa ujenzi madarasa 6

Na Judith Ferdinand, TimesMajira,Online Mwanza

MKUU wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masalla, amewapongeza wananchi wa Lukobe na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula kwa kufanikisha ujenzi wa madarasa sita ya shule mpya ya sekondari iliopo Masanza Mtaa wa Lukobe Kata ya Kahama, wilayani humo.

Masalla ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na wananchi wa Lukobe Kata ya Kahama, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Shule ya Msingi Lukobe, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya awamu ya pili ya kata kwa kata wilayani humo.

Ziara hiyo inalenga kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo, kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO-19,kusikiliza kero na changamoto za wananchi na kisha kuzipatia ufumbuzi,uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Buswelu.

Amesema katika ujenzi huo wa madarasa sita wananchi wametoa sh. milioni 17, huku Mbunge Dkt.Angeline akichangia matofali 3,000.

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masalla,akizungumza na wananchi wa Lukobe Kata ya Kahama,katika mkutano wa hadhara uliofanyika shule ya msingi Lukobe,ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya awamu ya pili ya kata kwa kata wilayani humo. Picha na Judith Ferdinand.

“Katika ujenzi huu niwapongeze sana wana Lukobe i wa viwango vikubwa,nampongeza Mbunge kwa kutoa tofali,”amesema Masalla.

Pia ametoa wito kwa Mkurugenzi na Ofisa Elimu,washiriane wote pamoja naye kumaliza miundombinu hiyo ili wasiwaweke watoto katika madarasa yasiyokuwa na hali nzuri, kwani wameona hali ya msongamano kwenye shule ilivyo kubwa.

Sanjari na hayo, alisema zamani wilaya hiyo ilikua inapokea kiasi cha sh. bilioni 1, katika sekta ya barabara lakini sasa wanapokea zaidi ya sh. bilioni 3,hivyo alimshukuru na kumpongeza Rais.

Aidha amesema, changamoto nyingine alioina ni muda wa kutoa maji,hivyo urekebishwe.