January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi Jimbo la Mbinga Mjini wafurahishwa na kasi ya maendeleo yanayoletwa na Mbunge Jonas

Na Mwandishi wetu ,Mbinga

Pamoja na Fursa nyingi za kiuchumi ambazo jimbo la Mbinga mjini limejaliwa ,bado lilikuwa linakabiliwa na Kero sugu ya maji na miundo mbinu ya Barabara hasa za vijijini ambazo zilihitaji mwakilishi ambaye ni mfatiliaji zaidi .

Jonas Mbunda ,anatajwa kuwa ni Mbunge ambaye ameweza kutatua kero sugu japo sio zote kwa kipindi kifupi , tayari ametekeleza ahadi nyingi alizotoa kwa wananchi wakati wa uchaguzi mkuu wakimchagua atahakikisha anazifanyia kazi haraka na kurudisha tabasamu

Wananchi wa kada mbalimbali jimboni , wanamzungumzia Mbunda kwa namna mbalimbali, mradi tu, wanamshukuru kwa utumishi na uwakilishi uliotukuka alioufanya kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali kutekeleza miradi ya maendeleo jimboni humo, samabamba na kuimarisha huduma za kijamii zikiwamo hasa huduma za Maji safi , Miundo mbinu, afya na elimu wakisisitiza kuwa, akujuaye na kukutakia uzima ndiye nduguyo maana afya ni mtaji.

Godfrey Kayombo amesema, kazi inayofanywa na Mbunge huyo ni kubwa kwani amekuwa akijitoa kwa hali na mali ilikutatua kero za wananchi wake, binafsi namuimba sana Radhi kwani sikumuunga mkono ila nimeelewa kwanini watu wengi wanampenda kwani anapenda sana maendeleo na nimfatiliaji sana inapokuja swala la maendeleo.

Grace Madereke amesema, Mbunge wa kwanza ambaye ametimiza ahadi zake kwa asilimia 95 tulikuwa na tatizo la maji sasa yapo ya kutosha amesimamia miradi ya uviko 19 kwa asilimia 95 kero ya barabara Tarura sasa wameanza matengenezo lakini amekuwa karibu sana na wananchi waliomchagua .

Amesema,kwa kweli akimaliza tu bunge siku ya pili yupo jimboni kwake kitu ambacho tulikuwa tukikitamani kwa siku nyingi simu za wananchi na viongozi hupokea kwa haraka na hutatua tatizo kama lipo ndani ya uwezo wake .

Emmanuel Mhagama amesema , kilio cha wananchi wa mbinga ilikuwa ni kero kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji lakini kwa sasa wanashukuru wamepata kiongozi mfatiliaji ambaye anayajua matatizo ya watu wake kwani amekuwa akisikiliza kero za wananchi mara kwa mara kwenye ziara zake na kuzitatua .

“Ni kiongozi mfatiliaji, mkarimu na anayependa kuona kero zote zinatatulika ni kiongozi wa kipekee ambaye mapenzi yake kwa wananchi wake, ni ya wazi, yasiyofichika na yanayogusa hisia za wote wanawake kwa wanaume; wazee kwa vijana; wadogo kwa wakubwa; maskini kwa tajiri; wasomi kwa wasiosoma mradi tu, na kiongozi anayepigania ustawi kwa watu wake wote”amesema Ngwenya .

Amesema: “Kwa kweli ni kuingo kizuri sana katio ya wananchi wa Mbinga , viongozi na serikali; anayependa kuona kero zikitatuliwa haraka na kwa njia bora zaidi.”

Naye Paul Halai mkazi wa Mbinga amesema, Kero ya maji kwa kata baadhi kama Mpepai ,Kilimani na Mbinga mjini hapa kwa kiasi kikubwa amesaidia Sana

Pia ameweza kusaidia kuleta husuma ya .Mtandao wa simu kwa kata ya MpepaiKusimamia barabara kukarabatiwa kwa baadhi ya barabara. Mbambi mateka, Betherehemu Utiri na Mbangamao Mpepai ,Kiwango cha lami Mbambi Matarawe

Aliyekuwa katibu wa CCM wa Wilaya ya Mbinga mjini Jacob Siay amesema, wananchi walikuwa wanataka Mbunge kama huyu ambaye yupo jirani nao na mpenda maendeleo ya kweli ,ambaye anafatilia kero zao na kujitoa bila ubaguzi.

Amesema, ili kujua kuwa Mbunge huyo ni chaguo sahihi la wananchi wa Mbinga mjini jaribu tu kumzungumzia vibaya kwa wapiga kura utachokipata utasahau ,kwani dhamana aliyoweka na anayoendelea kuweka ni kubwa sana kwa maendeleo ya wananchi wake.

Ameongeza “Anapenda kuona wananchi wanyonge wakiondokana na umaskini na badala yake, wanaingia katika maisha ya kawaida yaliyo bora na ndiyo maana amefanikiwa kutekeleza Ilani kwa asilia 97.

” huyu ndiye mwakilishi wa wananchi ambaye walikuwa wakimuhitaji , kwani ajaanza leo kuwasaidia wananchi alikuwa akiwasaidia hata kabla hajawa Mbunge, nimependa maendeleo na mchapakazi anajituma sana kuleta maendeleo ya wananchi , natutafika mbali kutokana na jitihada zake za maendeleo ,na ushirikishaji wananchi

“Kwa kweli mimi na chama changu hapa Mbinga tunajivuna kuwa na mbunge huyu mwanaume mpambanaji na anajua kero za watu wake anayeonesha nguvu na uwezo katika uongozi kwani ni wa kipekee na amekuwa akijitoa sana kusaidia wananchi wanyonge na hata chama.”

Kuhusu alivyochangia na kusaidia katika huduma Kinachovutia zaidi ni pale Mbunge alipotoa fedha zake za mfukoni ili kujenga vivuko viwili kwa kuchangia saruji na misumari hali ambayo imeongeza imani zaidi kwa wananchi wake.

Katibu wa CCM huyo wa Wilaya ya Songea mbinga amesema,amekuwa akitoa ushirikiano mkubwa kwa chama na amekuwa kiungo kizuri kati ya wananchi na serikali yao ni kiongozi wa mfano wa kuigwa.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Mbinga Mjini Jonas Mbunda amesema, tangu achaguliwe amejitahidi kufanya mikutano kila kata zaidi ya mara mbili ,pamoja na kufanya mikutano ya adhara ili kujua kero zinazowakabili ambapo ameweza kufanya ufatiliaji na kutoa msukumo wa ujenzi wa makorongo na madaraja hatarishi Kata ya Masumuni, Mikolola –Mbangamao, Mpepai na Kitanda,ameongeza msukumo ukamilishaji wa mradi wa maji Lusaka,Lifakara na Luwaita.

Amesema, kaweza kufatilia na kufanikisha ujenzi wa barabara ya Mbwalo la Mgambo – Mbuyula kiwango cha Lami kilometa 1, na barabara ya Mbuyula- Kipika kwa kiwango cha lami kilometa 1.Kukwangua barabara Mbalimbali za mji wa mbinga ambazo zilikuwa na changamoto ya kupitika ikiwemo barabara za Kata ya Mpepai, Mbangamao, Kikolo, Utiri, Mateka,Mbambi, Masumuni na Kagugu.

Aidha, alizungumza na RUWASA kupeleka mradi wa maji maeneo mbalimbali ya halmashauri ya mji Mbinga ikiwemo kata za Mpepai, Utiri, Kitanda ambapo kulikuwa na kero sugu ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

AFYA

Mbunge ametoa fedha na vifaa kutoka kwenye fedha ya Mfuko wa Jimbo na fedha binafsi kuboresha miundombinu ya Shule za msingi na Sekondari ndani ya Jimbo la Mbinga mjini.

Mbunge alitembelea ya Wilaya ya Mbinga (Mbuyula) kupokea changamoto zao na amekuwa akisemea suala la uchakavu wa Hospitali ya Mbuyula Bungeni na kwa Viongozi mbalimbali wanapofanya ziara Wilayani Mbinga,Serikali imeahidi kuendelea kutenga fedha kwaajili ya ukarabati wa hospitali hiyo.

Kata ya Utiri- Mbunge ametoa fedha ya Ringbeam na kuezeka Zahanati ya kijiji cha Mahande,Kata ya Mpepai- Mbunge ametoa fedha ya kununua bati kwaajili ya kuezeka Zahanati ya kijiji cha Mtua,Kata ya Mbangamao- Mbunge alinunua bati za kuezeka Zahanati ya kijiji cha Mikolola,

Kata ya Myangayanga- ametoa bati za kuezeka Zahanati ya kijiji cha MundekiKata ya Kilimani- Mbunge ametoa fedha za kununua bati kwaajili ya kuezeka Zahanati ya kijiji cha Rudisha,Kata ya Kikolo – Mbunge ametoa fedha za kununua bati kwaajili ya kuezeka nyumba (two in one) ya mganga na wahudumu wa zahanati ya Kata ya Kikolo.

Amesema, alifanya kikao na uongozi wa watu wenye ulemavu kupokea changamoto zao na kutoa maelekezo kwa Viongozi wa Idara ya Maendeleo ya jamii na Kitengo cha Ustawi wa Jamii kutoa huduma kwa usawa na kipaumbele kwa wahitaji bila kuwanyanyapaa ikiwemo katika mikopo ya halmashauri.

Mbunda amesema, alipeleka ombi maalumu Wizara ya Habari na mawasiliano kufuatia changamoto ya upatikanaji wa mtandao Kata ya Mpepai ambapo Mkurugenzi alimhakikishia kujengewa mnara wa simu na tayari Mnara wa wasimu mtandao wa AIRTEL umejengwa na kuzinduliwa mwezi January 2022.

Amesema kipaumbele chake cha kwanza ni kuhakikisha kuwa anawapigania wakulima wa kahawa ambao uchumi wao tangu 2017 umeyumba kutokana na serikali kuondoa makampuni kununua kahawa na kuleta sera ya ushirika hali ambayo imefanya maisha ya wakulima wa kahawa kuwa magumu zaidi tofauti na awali ,huku Mbinga iluwa inaongoza kwa uchumi imara na maendeleo mkoa wa Ruvuma.

Amesema atapigania na kusimamia Soko huria la kahawa ili wakulima wauze kahawa yao soko huria ilikuweza kujipatia kipato tofauti na sasa.”kipaumbele cha pili ni Afya nitahakikisha nasaidia na serikali itakayokuwa madarakani kuhimarisha huduma za afya hasa hospitali ya wilaya hususani huduma ya afya ya Mama na mtoto kwa kuweka miundombinu safi ya maji na pia kuimarisha huduma za uzazi kwani ssa hali ni mbaya na wanaita wodi ya wazazi machinjio , nitahakikisha serikali inawawajibisha wauguzi na madaktari wazembe ilikupunguza vifo vinavyotokana na uzembe,”amesema.

Amesema kilichomsukuma kuomba nafasi ya ubunge ni kutaka kushirikiana na wananchi wa jimbo la mbinga mjini na serikali itakayokuwa madarakani kutatua changamoto zinazowakabili kwa kuwa anazifahamu.

Ametaja Changamoto alizopanga kuzitatua kwa kushirikiana na serikali ni kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kuinua wakulima katika kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa bora pamoja na kutafuta masoko. Kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula ilikujitosheleza kwa chakula na kuuza ziada pamoja na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi.

Amesema,amejipanga kushirikiana na serikali kutatua changamoto ya Miundo mbinu ya barabara na umeme hasa maeneo ya vijijini, Huduma ya afya zahanati na matibabu pia kuinua hadhi ya hospitali ya Wilaya Mbuyula. Huduma ya Elimu kwa kuongeza idadi ya walimu pamoja na kusimamia kutolewa kwa elimu bora.

“Pia wananchi wa jimbo la mbinga mjini wanaimani nami kwakuwa wanajua mwakilishi wao halali katika jimbo kwakuwa ni mkazi wa mbinga tofauti wa wawakilishi wengine ambao walikuwa ni wazawa lakini hawaishi mbinga‘“.Amesema Mbunda.

Aidha ameendelea kusisitiza kuwa ataendelea kutatua kero za wanambinga kwa kushirikiana na wananchi ,serikali na wadau wa maendeleo ambapo amewataka wananchi wa Mbinga kuendelea kumpa ushirikiano na kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuleta maendeleo zaidi kwenye jimbo hilo.