Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Arusha
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo april 14.2022 amesema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linapenda kuwashukuru wananchi kwa namna ya pekee wanavyoshirikiana na Jeshi lao kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ambapo imepelekea Mkoa wetu kuwa shwari kipindi chote kuanzia mwezi January hadi hivi sasa.
Aidha kutokana na ushirikiano huo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kuwakamata wahalifu mbalimbali katika mkoa wetu kupitia misako na doria ambazo zimekuwa zikifanyika katika kuhakikisha matukio ya uhalifu yanapungua ama kuisha kabisa.
ACP Masejo amesema Kama mnavyofahamu kuwa waumini wa dini ya kikristo wapo katika mfungo wa kwaresma na wiki hii kutakuwa na ibada mbalimbali mchana na usiku kwenye nyumba za ibada ambazo zitahitimishwa na sikukuu ya kukumbuka kufufuka kwa Yesu Kristo yani PASAKA.
Kamanda Masejo amesema Katika kuhakikisha sikukuu hiyo inasheherekewa kwa amani na utulivu, Jeshi la Polisi mkoani hapa limejipanga vyema kuimarisha ulinzi maeneo yote hususani nyumba za ibada, kumbi za starehe ambapo askari watakuwa katika doria za miguu, mbwa pamoja na magari.
ACP Masejo ametoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kukemea maovu kwa waumini kupitia nyumba za ibada ili kujenga Jamii iliyo starabika. Pia niwaombe wananchi kuendelea kutoa taatifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao kwani kwa kufanya hivyo Mkoa wetu utaendele kuwa shwari.
“Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawatakia sikukuu njema ya Pasaka”
More Stories
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo
Walimu elimu ya lazima watatakiwa kuwa wabobezi kwenye masomo wanayofundisha