May 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi Arusha wapatiwa elimu ununuzi, umiliki ardhi

Na Queen Lema, Timesmajira Online,Arusha

Wananchi zaidi ya 200 kutoka maeneo mbalimbali nchini wamepatiwa elimu sahihi ya matumizi na namna ya kumiliki ardhi pamoja na mbinu mbadala za kunufaika nayo.

Hayo yameelezwa na Estomih Samanga ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Estomih Samanga Real Estate iliopo Intel jijini Arusha wakati akizumgumza na waandishi wa hhabari ofisini kwake juu ya umuhimu wa kumiliki ardhi.

Amesema kupitia elimu hiyo wananchi waliweza kutambua mambo mbalimbali ambayo awali walikuwa hawayajui.

“Unajua kuna mtu hajui kuwa ardhi ni hazina ambayo inalipa na kupanda gharama siku baada ya siku,lakini ardhi ni mtaji unapokuwa na ardhi yako unaweza hata kuaminika na taasisi nyingine za kifedha,”.

Pia amesema, elimu hiyo imeweza kuwasaidia wananchi kutambua aina ya udongo mzuri wa kujengea kwani kwa sasa wapo baadhi ya wajenzi ambao wanajenga nyumba lakini baada ya muda mfupi zinabomoka.

Hata hivyo amesema,kwa sasa wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma ya umiliki wa ardhi kwa njia rahisi ili kila Mtanzania aweze kujipatia ardhi .

“Ndani ya jamii kuna makundi mbalimbali tumeweka malengo ya kuhakikisha tunayafikia kwa njia rahisi na hivi karibuni tutafanya semina kwa wajasirimali wa sokoni,”.

Vilevile ametoa wito kwa vijana kutumia fursa ya njia ya kulipa kidogo kidogo ya kumiliki ili kurahisisha maisha ndani ya familia zao.