December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi 3000 wanufaika na matibabu bure kigamboni 

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online 

TAASISI ya Lions Club of Dar es Salaam Host kwa kushirikiana na LALJI FOUNDATION wameendesha kambi maalum ya matibabu ya bure ya siku tatu kwa wananchi wa wilaya ya kigamboni iliyofanyika katika hospitali ya vijibweni jijini dar es salaam ambapo imehusisha upimaji wa macho na magonjwa mbalimbali

Akizungumza wakati wa kambi hiyo mbunge wa jimbo la kigamboni Dkt Faustine Ndungulile amewataka wananchi kujenga tabia ya kupima afya mara kwa mara huku akibainisha kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Akizungumzia umuhimu wa kambi hiyo Rais wa Lions Club Dsm Host Mahmood Rajvani amesema kuwa lengo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwezesha matibabu ya macho ambayo mara nyingi yana gharama kubwa hususan kwa wananchi wa kipato cha chini.

Kwa upande wake mwenyekiti wa LALJI FOUNDATION Imtiaz Lalji amebainisha kuwa kambi hiyo imewafikia wananchi zaidi ya 3000 na kuwapatia matibabu ya macho bure huku akisisitiza kuwa afya ya macho ni muhimu katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo

Wananchi wa wilaya ya Kigamboni  waliojitokeza katika zoezi la upimaji wa macho bure wameeleza hisia zao kwa wanvyopitia changamoto kubwa ya ukosaji wa fedha ili kupata matibabu hayo.