December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanamwanza wahimizwa kutumia fursa za mikopo kuimarisha biashara

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Wito umetolewa kwa wanamwanza kutumia fursa za mikopo inayotolewa na taasisi za fedha ikiwemo benki ya NBC ili kuimarisha biashara zao.

Huku wafanyabiashara wakitakiwa kuunganisha nguvu kwa lengo la kufanikiwa kibiashara.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, katika hafla ya mazungumzo ya kibiashara na chakula cha jioni na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mwanza ilioandaliwa na National Bank of Commerce (NBC), iliofanyika jijini Mwanza.

Mhandisi Gabriel, amesema wanamwanza wafanye maandamano ya amani ya kiuchumi kwa kutumia fursa za mikopo kuimarisha biashara zao.

Pia amezihimiza taasisi za kifedha ikiwemo benki hiyo kupanua wigo wa huduma pamoja na kutoa elimu kwa jamii na wateja wao juu ya kuweka akiba,kukopa na kurejesha kupitia benki.
“Tuchangamkie fursa za mikopo kwa ajili ya kukuza biashara zetu,kwa maendeleo yetu na taifa letu, huduma zote zinazotolewa na benki hii ni kuanzia wajasiriamali wadogo,wa kati na wakubwa hivyo tuzitumie kikamilifu,”amesema Mhandisi Gabriel.

Akizungumzia hafla hiyo Mhandisi Gabriel,amesema ni taasisi chache zinazotoa nafasi ya kuendeleza mahusiano ya kibiashara na huduma huku wafanyabiashara watumie fursa hiyo kujenga mahusiano wao kwa waonkwa lengo la kufikia mafanikio zaidi.

“Niwapongeze NBC kwa jitihada za kuwaleta watu karibu nac kuwapatia fursa wateja wenu ya kutoa mrejesho ya kero mbalimbali wanazokutana nazo katika shughuli nzima ya kutoa huduma,”amesema Mhandisi Gabriel.

Awali akizungumza katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa idara ya wafanyabiashara wakubwa NBC makao makuu James Meitaron, ameeleza kuwa wanahuduma ya mikopo mbalimbali ikiwemo ya kusaidia wateja kujenga hususani majengo yanayohusiana na biashara wanazofanya ili kusaidia kuzalisha zaidi biashara zao.

“Katika hafla hii leo tumeungana na wateja wetu katika kufurahishana na kufahamishana kuhusu benki yetu na dhumuni ikiwa ni utekelezaji wa kauli mbiu ya NBC pia kutambulisha bidhaa na kupokea maoni,tunaendelea kutumia mfumo wa kidigitali ili kuwafikia wateja wetu zaidi nchini na sasa tuna matawi 47 na tutaendelea kuongeza zaidi, tuna mawakala nchi nzima wapatao 5,300 hii ikiwa ni kuwezesha malengo ya nchi nzima,”ameeleza Meitaron.

Sanjari na hayo ameeleza kuwa wamekuwa wakitoa huduma ambazo siyo za kifedha ambazo zimekuwa zikitolewa kwa wateja mbalimbali hususani wajasiriamali wadogo.

“Tunatoa mafunzo ya ujasiriamali kupitia klabu za biashara zinazoendeshwa na kufuatilia na NBC na tunazunguka nchi nzima ambapo mpaka sasa tumefanikiwa kuwafikia zaidi ya wajasiriamali 6090 ambayo yamejikita katika namna ya kupata huduma rafiki za kibenki,kuandaa mpango wa biashara na namna ya kufanya biashara,kukuza mtaji wao na tunawashauri wateja wetu waweze kukua kibiashara na kupata faida,”ameeleza Meitaron.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel,akizungumza katika hafla ya mazungumzo ya kibiashara na chakula cha jioni na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mwanza ilioandaliwa na National Bank of Commerce (NBC), iliofanyika jijini Mwanza.(Picha na Judith Ferdinand)
Mkurugenzi wa idara ya wafanyabiashara wakubwa NBC makao makuu James Meitaron, akizungumza katika hafla ya mazungumzo ya kibiashara na chakula cha jioni na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mwanza ilioandaliwa na National Bank of Commerce (NBC), iliofanyika jijini Mwanza.(Picha na Judith Ferdinand)

Baadhi ya wafanyabiashara mkoani Mwanza waliohudhuria katika hafla ya mazungumzo ya kibiashara na chakula cha jioni na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mwanza ilioandaliwa na National Bank of Commerce (NBC), iliofanyika jijini Mwanza. ya kibiashara na chakula cha jioni na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mwanza ilioandaliwa na National Bank of Commerce (NBC), iliofanyika jijini Mwanza.(Picha na Judith Ferdinand)
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel,akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa benki ya NBC na serikali pamoja na wafanyabiashara waliohudhuria katika hafla ya mazungumzo ya kibiashara na chakula cha jioni na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mwanza ilioandaliwa na National Bank of Commerce (NBC), iliofanyika jijini Mwanza. ya kibiashara na chakula cha jioni na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mwanza ilioandaliwa na National Bank of Commerce (NBC), iliofanyika jijini Mwanza.(Picha na Judith Ferdinand)