Na Mwandishi Wetu
YAUNDE, Ofisi ya Rais wa Cameroon imekiri kuwa wanajeshi watatu walishirikiana na wanamgambo wenye silaha kuwaua raia 23 ikiwemo watoto 10 katika jimbo lenye wakazi wanaozumngumza Kiingerereza ndani ya Kijiji cha Ntumbo mwezi Februari, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyosomwa kupitia redio ya taifa ilieleza kuwa, wanajeshi watatu na wapiganaji wa kundi la waasi walivamia kambi moja ya jeshi na kuwaua watu hao kabla ya kuchoma moto eneo hilo kuficha ushahidi.
Awali, Serikali ya Cameroon iliyapinga madai ya kuhusika na mauaji hayo kwenye jimbo ambalo wapiganaji wanaotaka kujitenga kwa jamii ya wanaozungumza kiingereza wanapambana na vikosi vya Serikali kwa miaka miwili.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mauaji hayo ya raia yalitokea usiku wa Februari 13 katika kijiji cha Ntumbo, Ambazonia.
Hapo kabla jeshi la Cameroon lilidai vifo vya watu hao vilitokana na ajali ya moto wakati wa mapambano na wanaotaka kujitenga.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria